Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza Dylan Kerr kwa kocha wa makipa Idd Salim (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. |
KOCHA mpya wa Simba, Muingereza Dylan Kerr amesema ataendeleza wachezaji chipukizi ili kuwa na timu bora kwa sasa na baadae.
Kerr aliyasema hayo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na wajumbe wa Kamati ya Simba, Collin Frisch na Said Tully.
“Nimefurahi kuja Tanzania na nawaahidi viongozi na mashabiki kuwa nitahakikisha naendeleza wachezaji chipukizi hili Simba iweze kutamba sasa na baadae”, alisema Kerr.
Kocha huyo ambaye amerithi mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba ambapo atakuwa anasaidiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Suleman Matola.
Wakati Kerr akiwasili pia alikutana na kocha mpya wa makipa Idd Salim toka Kenya ambaye naye aliwasili tayari kwa kazi yake mpya kwenye klabu ya Simba.
Simba waliamua kuachana na Kopunovic na kusaka kocha huyo mpya baada ya Mserbia huyo kuhitaji Simba imlipe kiasi cha Dola za Marekani 50,000 (sh. Milioni 100) kama ada ya usajili na mshahara wake ambapo kila mwezi atakuwa analipwa dola za Marekani 14,000 9sh. Milioni 28).
Baada ya kushindwana kwenye malipo ndipo uongozi uliamua kumsaka kocha mpya na kumpata Kerr ambaye inasemekana atalipwa mshahara wa dola za marekani 9,000 sawa na milioni 18 kwa mwezi.
Kaka ukichukua kazi ya mtu mpe credit basi, si vizuri kukopi na kupaste bila kusema umetoa wapi.
JibuFuta