NEYMAR AFUNGIWA MECHI NNE NA FAINI MILIONI 20
MSHAMBULIAJI
Neymar hataonekana tena kwenye kikosi cha Brazil katika michuano ya
Copa America mwaka huu, baada ya kufungiwa mechi nne jana usiku.
Mpachika
mabao huyo wa Barcelona alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya mchezo
ambao Brazil walifungwa na Colombia mjini Santiago Jumatano.
Awali
alifungiwa mechi mbili, lakini Baraza la Soka Amerika Kudini (CONMEBOL)
limeamua kuitanua adhabu hiyo hadi kuwa mechi nne na pia kumpiga faini
ya dola za Kimarekani 10,000 (Sh. Milioni 20).
Pia
ilielezwa kwamba Neymar alimtolea 'maneno ya shombo' refa wa Chile,
Enrique Osses baada ya kumsubiri kwenye sebule ya kuelekea vyumba vya
kubadilishia nguo.
Nahodha
huyo wa Brazil, alitolewa kwa kadi nyekundu usiku wa kuamkiaa Alhamisi,
Brazil ikifungwa bao 1-0 na Colombia katika Copa America.
Nyota
huyo wa Barcelona alipiga mpira kuelekeza kwa mchezaji wa Colombia,
Pablo Armero baada ya mechi kabla ya kutaka 'kumfanyizia' na mfungaji wa
bao, Jeison Murillo.
Pamoja na hayo, refa Enrique Osses hakuwa na namna zaidi ya kumuonyesha Neymar kadi nyekundu ya moja kwa moja, adhabu ambayo pia alimpa mshambuliaji wa Colombia, Carlos Bacca ambaye alianzisha vurugu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, mara moja alikiri kufanya makosa - lakini hakutaka kuomba radhi. "Nilikuwa
nina ishu na mmoja wa mabeki wao.
Ni kwamba alikuwa ana ishu na mimi,
mchezo ulipomalizika na niliposikia kipyenga - nikaupiga mpira na kwenda
kumpiga mchezaji wa Colombia. Kisha beki wao akataka kuzinguana na
mimi, nikamuangalia tu.
"Nimefanya
kosa. Lakini ni sehemu ya mchezo, tumefungwa na tumecheza vibaya.
Sikucheza vizuri pia. Nakiri hilo na kuwajibika kwa kilichotokea leo. Sikimbii. Sasa ni juu yetu kushinda mchezo ujao,"amesema mchezaji huyo wa Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni