PLUIJM ATUA KUANZA MAJUKUMU YA KUINOA YANGA
Kocha
mkuu wa klabu ya Yanga Hans van der Pluijm tayari ameshawasili jijini
Dar es Salaam akitokea nchini Ghana alikokuwa kwa mapumziko mara baada
ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu Tanzania bara 2014-2015 ambapo
alikiongoza kikosi cha wanajangwani kutwaa ubingwa wa ligi.
Pluijm
amerejea kuanza majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga kwa ajili ya
michuano mbalimbali inayoikabili timu hiyo ikiwa ni pamoja na mashindano
ya Kagane Cup, ligi kuu Tanzania bara na ile ya vilabu bingwa barani
Afrika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni