STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 3 Juni 2015

RAFAEL BENITEZ ASAINI MIAKA 3 REAL MADRID

Rafa Benitez atambulishwa kuwa Kocha mpya wa Klabu ya Real Madrid leo, Asaini Mkataba wa miaka 3.

Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 55, ambaye anarejea kwenye klabu aliyojifunzia ukocha kama kocha wa timu ya vijana na kupata leseni C akiwa mchezaji, alikuwa na mkewe Montse wakati akitambulishwa na Rais Florentino Perez mbele ya Wakurugenzi na Waandishi wa Habari. 

Perez alisema: "Tunashawishika kuwasili kwa Benitez kutatufanya tuwe wa nguvu. Tunamleta kocha ambaye wakati ametaka kuwa kocha wa klabu hii. Mtu fulani mmoja ambaye anafahamika kwa juhudi zake na utaalamu,".

Perez alisoma orodha ya mataji ambayo Benitez amewahi kushinda katika timu alizofundisha likiwemo la Ligi ya Mabingwa alilolitwaa akiwa na Liverpool na mawili ya La Liga aliyochukua alipokuwa Valencia. 

Akasema: "Anaifahamu hii klabu. Ni mmoja wetu. Alifika hapa akiwa na umri wa miaka 13 na nafikiri ni maalum sana kwake kupewa timu kama kocha leo. Mpendwa Rafa, karibu nyumbani.’

Benitez alitambulishwa kama kocha mpya wa Madrid katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo baada ya ziara ya kutembezwa katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Valdebebas. 

Alipata fursa ya kusalimiana na kocha gwiji wa klabu, Iker Casillas, ambaye inasemekana mikoba yake kama kocha namba moja wa Hispania na Real Madird itarithiwa na David De Gea msimu ujao.

"Leo si siku ya kuzungumzia masuala binafsi. Nataka kufurahia vipaji vikubwa navyokwenda kukutana navyo katika timu,".

Na badaye alipoulizwa; "Unafikiri nini kuhusu Casillas kama kipa?’ akarudia alichosema; "NImesema kabla, sifikiri nitazungumzia kuhusu mchezaji mmoja mmoja na hata kujibu swali hili,".

WASIFU WA RAFA BENITEZ 

Kuzaliwa: Aprili 16, 1960
KLABU ALIZOCHEZEA
Real Madrid Castilla (1974-1981), Parla (Mechi 124 za Ligi, 1981-1985), Linares (Mechi za 34 ligi, 1985-1986). 
TIMU ALIZOFUNDISHA
Real Madrid B (1993–1995), Valladolid (1995–1996), Osasuna (1996), Extremadura (1997–1999), Tenerife (2000–2001), Valencia (2001–2004), Liverpool (2004–2010), Inter Milan (2010-2011), Chelsea (2012–2013), Napoli (2013–2015), Real Madrid (2015–present)
MATAJI ALIYOSHINDA
VALENCIA
La Liga: 2001–02, 2003–04; UEFA Cup: 2003–04
LIVERPOOL
Kombe la FA: 2005–06; Ligi ya Mabingwa Ulaya: 2004–05; Super Cup: 2005
INTER MILAN
Super Cup ya Italia: 2010; Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA: 2010
CHELSEA
Europa League: 2012–13
NAPOLI
Coppa Italia: 2013–14; Super Cup ya Italia: 2014

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox