STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Juni 2015

SIMBA SC YALETA MZUNGU MWINGINE. KAZI IPO SAFARI HII

Katika mkakati endelevu wa kuboresha benchi la ufundi, Klabu ya Simba imeingia mkataba na Dušan Momčilović kama kocha mpya wa mazoezi ya viungo na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
Kocha huyo kutoka Nchini Serbia ana uzoefu mkubwa katika fani ya mpira wa miguu hususani mazoezi ya viungo. Kocha Dušan amefundisha klabu mbalimbali duniani kwenye Nchi kama Malaysia, Indonesia, Georgia ambako Alikuwa kocha wa mazoezi ya viungo wa klabu ya FC DINAMO ambayo ilicheza mechi za awali ya klabu bingwa ya Ulaya-UEFA, Bosnia and Herzegovina, Oman na Belgrade
Kocha Dušan pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu ya FC SOGOR –Tobruk – Libya.
Kocha Dušan ni muhitimu wa Digrii ya Mazoezi ya Viungo jijini Belgrade akiwa amejikita Zaidi kwenye mazoezi ya viungo na kujenga mwili.
Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha Dušan Momčilović mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox