STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 29 Juni 2015

STUTTGART YASAJILI GOLIKIPA WA DORTMUND.

KLABU ya Stuttgart imefanikiwa kumsajili golikipa Mitchell Langerak kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka kwa mahasimu wao Bundesliga Borussia Dortmund. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Australia mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na Dortmund akitokea Melbourne Victory mwaka 2010 na kufanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza Februari mwaka uliofuata wakati Dortmund walipotandikwa mabao 3-1 na Bayern Munich. Msimu uliopita Langerak ambaye alikuwa golikipa namba mbili wa Dortmund alicheza mechi tisa za Bundesliga. 

Langerak amelazimika kuondoka baada ya meneja mpya wa Dortmund Thomas Tuchel kumleta Roman Burki kutoka klabu ya Freiburg mapema mwezi huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox