STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 1 Julai 2015

BLATTER HATOHUDHURIA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE 2015

BLATTER HATOHUDHURIA FAINALI YA KOMBE LA DUNIA LA WANAWAKE 2015



Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) Sepp Blatter hatohudhuria kwenye mchezo wa fainali wa kombe la dunia la wanawake 2015 mchezo utakaopigwa Vancouver, British Columbia, Blatter hatohudhuria fainali hiyo kutokana na sababu zake binafsi.

Kiutamaduni, rais wa FIFA ndiye anaetakiwa  akabidhi  kombe la dunia kwa mshindi wa fainali hiyo ya wanake, lakini mwaka huu haitakuwa hivyo. Imeripotiwa na shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba, mwanasheria mkuu wa FIFA Richard Cullen amethibitisha habari hizo akisema:

“Hatokuwepo kwenye mchezo wa fainali Canada. Amewataarifu waratibu wa michuano hiyo na amesema ana sababu zake binafsi za kutohudhuria”.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kutokea tangu Blatter aanze kuiongoza FIFA kutohudhuria sherehe za fainali za kombe la dunia. Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo Ker Radnedge, katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke pia hatokuwepo Canada.

FIFA imesema sababu za kutokuwepo kwao ni kutokana na wote kuakabiliwa na majukumu huko Zurich.

Blatter amethibitisha atajiuzulu nafasi yake ya urais wa FIFA baada ya uchunguzi wa maafisa wa Kimarekani kubaini kuwepo na sakata la rushwa ndani ya FIFA na kuwakamata baadhi ya maafisa wa shirikisho hilo.

Mwandishi wa The Guardian Owen Gibson amehoji kwamba, Tangu uchunguzi huo uwekwe hadharani, Blatter amekuwa hasafiri tena mara kwa mara, ni rahisi kujua ni kwanini.
Blatter fear

Gibson ameripoti kwamba, Blatter pia anafanyiwa uchunguzi na shirika la Kimarekani la FBI akituhumiwa kwa matukio ya rushwa na ubadhilifu wa pesa yanayo ikabili FIFA lakini mamlaka za Uswis tayari zimethibitisha kwamba, Blatter hayupo kwenye watu wanaofanyiwa uchunguzi na mamlaka hizo.

Watu wengi wamekuwa wakisema kuwa, Blatter huenda anahofia kukamatwa pindi atakapo safiri kwenda Canada. Lakini kutokuwepo kwake kwenye fainali ya kombe la dunia la wanawake hakutatoa picha nzuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox