STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 5 Julai 2015

CAFU ADAI BRAZIL HAIOGOPWI KAMA ZAMANI.

BEKI wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Cafu anaamini taifa hilo limekuwa haliogopewi tena na wapinzani wao baada ya kutolewa nje katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Copa America. 

Brazil walitolewa katika michuano hiyo ya nchi za bara la Amerika Kusini kwa matuta na Paraguay ikiwa imepita mwaka mmoja baada ya kusasambuliwa mabao 7-1 katika ardhi yao na mabingwa wa Kombe la Dunia Brazil. 

Cafu ambaye amewahi kushinda mataji mawili ya Kombe la Dunia na Copa America katika kipindi cha miaka 16 aliyocheza soka anaamini vipigo hivyo sio vimeondoa hali ya kujiamini kwa wachezaji lakini pia kutoogopewa tena katika soka na mataifa mengine duniani. 

Cafu amesema Brazil wamekosa ari na moyo wa kujituma katika soka na sasa wanacheza na wapinzani ambao hawaahofii tena kama ilivyokuwa zamani. 

Hata hivyo, Cafu aliendelea kudai kuwa Brazil inapita katika kipindi cha mpito kwasasa lakini watakuja tena kutawala soka na kuwafanya wapinzani kuwahofia tena huku wale wanaowaponda wakishangazwa na mabadiliko hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox