STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 21 Julai 2015

GOR MAHIA WATAJA BEI YA OLUNGA,SIMBA,YANGA NA AZAM WAJIPANGE

Mshambuliaji hatari wa timu ya Gor Mahia na timu ya Taifa ya Kenya,  Michael Olunga baada ya jana kutupia goli mbili wakati timu yake ikicheza na KMKM na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 3-1, amesema kuwa bado kikosi chao kina kazi nzito ya kufanya  licha ya kufanya vizuri mechi mbili za kwanza.
Olunga amesema lengo lao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Kagame na kama wanataka kufanya hivyo basi wanatakiwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano hayo yanayoshirikisha vilabu bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Olunga ameingia kwenye rada za miamba ya kandanda Tanzania, Simba, Yanga na Azam  FC.
Tetesi zinasema kwamba Yanga na Azam wanaitaka saini ya nyota, huku Simba wakithibitisha kwamba wametenga dola Elfu 20 kumsajili mkali huyo wa kucheza na nyavu.
Hata hivyo viongozi wa Gor Mahia wanasema kwamba timu inayotaka huduma ya Olunga inatakiwa kutoa dau la dola elfu 50 kwa klabu hiyo ili kuvunja mkataba, halafu wakae na mchezaji kujua anataka Shilingi ngapi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox