STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 20 Julai 2015

MOURINHO KUVUNJA BENKI KWA KITASA HIKI


Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho  anamtaka kwa nguvu zote John Stones katika uwanja wa Stamford Bridge.

Mourinho anamuona mlinzi huyo wa Everton kama mrithi wa nahodha wa muda mrefu wa The Blues, John Terry na yuko tayari kuvunja benki ili kupata huduma yake.
Kocha wa Everton, Roberto Martinez  anaweka ngumu kuuza 'chombo' hicho cha maana, lakini Mourinho amekomaa naye.
The Guardian wameripoti kwamba Chelsea wapo tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa beki huyo wa England ili kumshawishi Martinez.
Mwaka 2002, Rio Ferdinand alisajiliwa na Manchester United kutoka Leeds kwa dau la paundi milioni 30 na mpaka sasa anabakia kuwa mlinzi ghali zaidi katika historia ya soka la England.
Everton tayari wamekataa ofa ya paundi milioni 20 na Chelsea wanajaribu kuwashawishi kwa paundi milioni 26, wakikataa, Mourinho anaongeza mzigo mwingine mpaka kieleweke.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox