STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 17 Julai 2015

HII NDIYO VIDEO YA KOMBE LA DUNIA 1950 MAREHEMU GHIGGIA AKIWA SHUJAA





Baada ya kombe la dunia 1938 kufanyika mipango ikawa ni maandalizi ya kombe la dunia 1942  lakini kutokana na vita vya dunia vya pili  kombe la dunia halikuweza kuchezwa vilevile 1946 halikufanyika 1950 Brazil wakapewa uwenyeji baada ya hali ya mambo kuwa tulivu Duniani.

Fainal zikawa timu zote za amerika ya kusini  wenyeji Brazil dhidi ya Uruguay
ndani ya dimba la Maracana-Rio de Janeiro ambalo lilikuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji  199,854.

Mtanange uliteka hisia kubwa huku wa brazil wakiwa na imani kubwa kutwaa ubingwa huo walifurika ndani ya maracana  takribani mashabiki 205,000 wakahudhuria mchezo huo ambapo wingi huo ni rekodi lakin pia ulipitiliza idadi iliyotakiwa ktk uwanja ya mashabiki 199,854.

 Mwamuzi akiwa ni George  Reader wa Uingereza mnamo dakika ya 47 Brazil 
 wakawa wa kwanza kufunga kupitia  Albino Friaca Cardoso winga wa Sao Paulo wakati huo,  lakini dakika ya 66 Juan Alberto Schiaffino Villano wa Uruguay akasawazisha.


Dakika ya 79 Alcides Edgardo Ghiggia akaipatia Uruguay goli la pili na la ushindi na kuwaacha wabrazil wakiduwaa kwa kushindwa kuchukua kombe la dunia ndani ya dimba la nyumbani.

 Hiko ndicho tulizungumza kwenye sports details siku ya jana kwenye kumbukumbu za michuano hiyo Taarifa kutoka nchini Uruguay zinasema Alcides Edgardo Ghiggia mchezaji pekee aliebakia hai katika kikosi kilicho cheza 1950 amefariki Dunia akiwa na miaka 88 wakati ambao Uruguay inakumbuka miaka 65 tangu awatoe kimasomaso katika dimba la Maracana nchini Brazil.

Ukiachilia mbali tukio hilo la kukumbukwa pia wanamichezo wengi watamkumbuka kwa kauli yake kuwa " ni binadamu watatu tu waliofanikiwa kuunyamazisha uwanja wa Maracana ni yeye mwenyewe, Papa na mwanamuziki Frank Sinatra.

Image result for GHIGGIA
6

Image result for GHIGGIA
        
                                              








                                         R.I.P-GHIGGIA




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox