STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 22 Julai 2015

MASHABIKI WATWANGANA HADHARANI

MASHABIKI wa Leeds United wamepewa mkong'oto na mashabiki wa Eintracht Frankfurt usiku wa jana baada ya mchezo wa kirafiki baina ya timu hizo  uliofanyika Austria.

Polisi mjini humo wamewashutumu mashabiki wa timu ya Ujerumani kwa kuanzisha vurugu, ambazo zilisababisha watu 25 wakamatwe na wengine kibao kuachwa wanavuja damu kwa majeraha.



Taarifa kutoka katika eneo la tukio, zinasema kwamba kundi la mashabiki 100 wa Frankfurt baadhi yao wakiwa wamevaa vitu vya kuficha sura zao, liliwavamia kundi la mashabiki wa Leeds uwanjani baada ya Wajerumani kushinda 2-1. 


Riot police attempt to control rival supporters as they fought on the pitch after the final whistleMara tu baada ya mechi mashabiki wa timu hizo walianza kutupiana makonde na mateke uwanjani mjini Eugendorf, karibu na Salzburg.

Mashabiki watatu wa Leeds, Maofisa wawili wa Polisi na walinzi wa uwanjani walipelekwa hospitali kwa matibabu. Inaaminika kwamba 17 kati ya waliokamatwa walikuwa mashabiki wa Frankfurt.

Polisi ilitumia mabomu na mbwa kuwatawanya mashabiki hao waliokuwa katikati ya mpambano mkali.

A bloodied Leeds United fan receives treatment in the car park at the stadium in Eugendorf, near Salzburg in Austria
Shabiki huyu wa Leeds United alikuwa mkong’oto wa nguvu na kuvuja damu 
















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox