STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 4 Julai 2015

STARS YAJITITIMUA YATOA SARE YA 1-1 NAKIVUBO



TANZANIA imetupwa nje ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya sare ya 1-1 jioni ya leo Uwanja wa Nakivubo, Kampala, Uganda.

Matokeo hayo yanamaanisha, Stars imetolewa kwa kipigo cha jumla cha mabao 4-1, baada ya awali kufungwa 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Raundi hiyo ya kwanza visiwani Zanzibar wiki mbili zilizopita.

Dakika 45 za kwanza zilimalizika kukiwa hakuna timu iliyopata bao na kipindi cha pili na kipindi cha pili, John Bocco ‘Adebayor’ alianza kuifungia Tanzania kwa penalti dakika ya 53 kwa penalti.

Penalti hiyo ilitolewa baada ya beki wa Uganda kuunawa mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Tanzania, Rashid Mandawa.

Uganda walifanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika za lala salama kupitia Robert Sentongo  baada ya mabeki wa Stars kutegeana  kuondosha mpira na kwa matokeo hayo Uganda   wanasonga mbele katika mbio za CHAN ya mwakani nchini Rwanda. 

Matokeo haya ya sare baada ya vipigo vitano mfululizo kwa Stars yanakuja chini ya kocha mpya, Charles Boniface Mkwasa kufuatia kufukuzwa kwa Mholanzi, Mart Nooij baada ya kufungwa na Uganda 3-0 Zanzibar.

Kikosi cha Uganda kilikuwa; James Alitho, Denis Okot Oola, Brian Ochwo, Hassan Waswa Mawanda, Shafiq Bakari, Derick Tekkwo, Muzamil Mutyaba, Erisa Sekisambu, Farouk Miya, John Semazi na Robert Sentengo.












Tanzania; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo/Said Ndemla, John Bocco, Rashidi Mandawa na Simoni Msuva/Ramadhani Singano ‘Messi’.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox