MSHAMBULIAJI mpya wa Manchester City, Raheem Sterling amefanikiwa kufunga bao dakika tatu katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya AS Roma uliochezwa katika Uwanja wa MCG jijini Melbourne leo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, amejiunga na City kwa kitita cha paundi milioni 49 kutoka Liverpool Julai 14 mwaka huu.
Sterling alikuwa akicheza akitokea upande wa kushoto sambamba na washambuliaji wengine wawili akiwemo David Silva na chipukizi Kelechi Iheanacho, kabla ya kutolewa katika muda wa mapumziko.
Iheanacho pia alifunga bao katika mchezo huo ambao City walishinda kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.
Mchezo huo ni wa kwanza kwa City katika michuano ya Kimataifa ya Kirafiki ambapo sasa watachuana Real Madrid Ijumaa hii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni