STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 1 Julai 2015

WOLFSBURG YADAI HAWANA MPANGO WA KUMUUZA DE BRUYNE.

WOLFSBURG YADAI HAWANA MPANGO WA KUMUUZA DE BRUYNE.




MKURUGENZI wa michezo wa Wolfsburg, Klaus Allofs amesisitiza kuwa klabu hiyo haina mpango wowote wa kumuuza Kevin De Bruyne katika usajili wa majira haya ya kiangazi.

Manchester City ndio wanaonekana kumuwinda nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji huku mwenyewe akithibitisha mapema mwezi huu kuwa wakala ameshafanya mazungumzo na klabu hiyo.

Hata hivyo, Wolfsburg bado wameendelea na msimamo wao wa kutotaka kumuacha De Bruyne na Allofs amebainisha kuwa klabu hiyo inatarajia kuangalia uwezekano wa kumboreshea maslahi katika mkataba wake nyota huyo mwenye umri wa miaka 24.

 Allofs amesema De Bruyne ana mkataba na Wolfsburg unaomalizika mwaka 2019 na tayari wameshatuma ujumbe kuwa hawana mpango wa kumuuza. Mkurugenzi huyo aliendelea kudai kuwa kikubwa wanachotizama hivi sasa ni kupitia upya mkataba wake na kuangalia jinsi ya kuuboresha zaidi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox