Mechi
ya raundi ya kwanza ya kombe la Ujerumani baina ya timu za daraja la
chini ilivunjika kipindi cha pili kufuatia mwamuzi kupigwa na kitu
kutoka kwa mashabiki.
Refa huyo, Martin Petersen hakuumia sana, lakini alizipeleka timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo dakika ya 71.
Wakati
huo, wenyeji Osnabrueck, ambao hucheza ligi daraja la tatu walikuwa
wanaongoza 1-0 dhidi ya RB Leipzig ya daraja la pili.
Refa alizitoa timu uwanjani dakika ya 71
Osnabrueck walifunga goli lao katika sekunde ya 23.
Chama cha soka cha Ujerumani (DFB) kimeanza uchuguzi wa tukio hilo.
Refa akisikilizia maumivu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni