Msimu uliopita wa ligi kuu ya Uholanzi, Eredivisie, Memphis Depay alimaliza mfungaji bora wa mabingwa PSV.
Depay alikuwa anacheza winga ya kushoto na aliposajiliwa Manchester United, mashabiki walitegemea kumuona anacheza nafasi hiyo.
Pia aliimudu vyema nafasi hiyo akiichezea timu ya Taifa ya Uholanzi, akipiga pasi za mwisho na krosi murua.
Lakini mechi ya Jumamosi ya
ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Tottenham, Depay alianzishwa namba 10 na
kuzua kelele kwa mashabiki wa United.
Nyota huyo mpya wa Manchester
United anayevalia jezi namba 7 hakuonesha kiwango kikubwa, alionekana
kama samaki ndani ya maji, hakuonesha ufundi wake wa kuchezesha safu ya
ushambuliaji kama alivyozoeleka.
Kocha wa United, Louis van Gaal
ameweka wazi sababu ya kumchezesha Memphis namba 10 ambayo inaonekana
kama ya ajabu: ni kwasababu ya Ashley Young.
Young ameanza vizuri msimu
chini ya Van Gaal na nyota huyo anaonekana kushikilia hatma ya Man
United, hivyo ni ngumu kwa Memphis kuchukua nafasi yake.
Van Gaal anahisi Memphis alifanya vizuri katika nafasi ya namba 10, lakini anaamini ni ngumu kumtoa Young.
“Ni nafasi mpya kwake, anatakiwa kuizoea kwasababu ni mfungaji mzuri”.
“Tusubiri kuona kama ataweza kukidhi haja ya namba hiyo, lakini hii
ni kwasababu Young anacheza vizuri sana winga ya kushoto. Haya ndiyo
mazingira, ila naweza kubadili katikati ya msimu na akacheza nafasi
hiyo”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni