TAREHE
ya mwisho ya kufunga dirisha la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, imesogezwa tena mbele hadi Agosti 30 kwa ada ya Sh. 500,000 kwa
kila mchezaji.
Lakini klabu ambazo zitakamilisha usajili wa wachezaji wake Agosti 20, hazitalipwa fedha hizo.
Taarifa
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kwamba baada ya awali
kusogeza dirisha hilo kutoka Agosti 6, hadi 20, baada ya muda huo klabu
itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki
tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya Agosti
30.
Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6 Septemba.
Kikao cha kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.
Kuanzia tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza (FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni