mshambuliaji
wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesikia ushindi wa Simba kwenye michezo
sita ya kirafiki huku akifuatilia rekodi za straika Hamis Kiiza na
kutamka kuwa kama hatapewa ushirikiano ni lazima achemshe Msimbazi.
Akizungumza
na Mwanaspoti, Niyonzima aliyewahi kucheza na Kiiza ndani ya Yanga,
alisema straika huyo anapata wakati mgumu sasa kutokana na kubadili
mazingira na itachukua muda kuyazoea, hivyo ni lazima Simba impe muda
kabla ya kuanza kumhukumu.
“Kiiza
ameenda Simba, huenda akapata tabu ya kuendana na staili ya uchezaji wa
Simba na kama akinyimwa ushirikiano atapotea kabisa.
“Simba
na Yanga zina falsafa tofauti ingawa mchezaji yeyote mzuri ataweza
kuendana na mpira wowote ule, cha msingi ushirikiano na kama hilo
litakuwepo, mtu kama Kiiza ataweza kutamba lakini kama hali itakuwa
tofauti, itamchukia na hatoweza kutamba,” alisema.
Alisema
lazima Kiiza apate mawinga wenye kasi, pia anahitaji timu impe nafasi
ya kufanya yake na kama timu itapiga pasi nyingi za taratibu mambo
huenda yakawa magumu kwake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni