Baba Rahman (kulia)
Chelsea imekubali kuilipa paundi milioni 21.7 klabu ya Augsburg ili imsajili mlinzi wake wa kushoto, Abdul Baba Rahman.
Mazungumzo
baina ya klabu hizo yamekuwa yakiendelea kwa wiki kadhaa, lakini sasa
makubaliano ya awali yanasema kwamba Chelsea watalipa paundi milioni 14
kabla ya kuongeza paundi milioni 3.5 kutegemea na kiwango chake,
wataongeza tena paundi laki 7 pale ambapo Rahman atafikisha mechi 20 na
kisha watamalizia paundi 3.5 baada ya kucheza mechi 100.
Nyota
huyo wa kimataifa wa Ghana amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na
anajiandaa kwenda London kupima afya kabla ya kutambulishwa rasmi kuwa
mchezaji wa Chelsea baadaye wiki hii.
Nyota huyo alikuwa katika rada za Manchester City, Arsenal na Roma.
Jose Mourinho ameamua kusaini beki mwingine wa kushoto
ili asaidiane na Cesar Azpilicueta baada ya Filipe Luis kurejea Atletico Madrid.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni