STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 6 Agosti 2015

KAMA KAWAIDA: USAJILI WASOGEZWA MBELE, SASA KUFUNGWA AGOSTI 20


WAKATI awali dirisha la usajili wa ligi lilikuwa lifungwe leo saa sita usiku, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limesogezwa mbele mpaka Agosti 20 mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto alisema dirisha la usajili wa wachezaji kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) sasa litafungwa  Agosti 20 mwaka huu.

Awali dirisha la usajili lilikua lifungwe leo , na usajili mdogo wa ndani ungefungwa Septemba 5, 2015 lakini sasa usajili wote kwa jumla utafungwa Agosti 20”, alisema Kizuguto.

Pia alisema Agosti  Agosti 21- 28 ni kipindi cha pingamizi, Agosti  29-30 ,Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itapitia na kupitisha usajili.
Dirisha la uhamisho wa wachezaji wa Kimataifa (FIFA –TMS) litafungwa Septemba, 6 na Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 12.

Aidha TFF inavitaka vilabu kukamilisha usajili huo katika muda uliowekwa, ili kupunguza usumbufu wa kufanya usajili dakika za mwisho,na dirisha litakapofungwa Agosti 20, litafunguliwa tena wakati wa dirisha dogo mwezi Novemba 15 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox