STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 16 Agosti 2015

MCHEZAJI WA CAMEROON ASAINI MIAKA MITANO TOTTENHAM HOTSPUR



Tottenham imetangaza kumsajili Mcameroon Clinton N'Jie kutoka Lyon kwa ada ya Pauni Milioni 10

WASIFU WA CLINTON N'JIE 

Kuzaliwa: Agosti 15, 1993
Ameicheza mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita 
Alijiunga na Lyon mwaka 2010 kwa msaada wa kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo, Jean-Jacques Nono. Novemba 2012 aliichezea mechi ya kwanza Lyon akitokea benchi timu ikishinda 3-0 dhidi ya Reims, kabla ya msimu uliopita kung'ara katika Ligue 1, akifunga mabao nane katika mechi 33 za mashindano yote 15 tu akianza. 
















KLABU ya Tottenham Hotspur ya Ligi Kuu ya England imethibitisha kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Cameroon, Clinton N'Jie kutoka klabu ya Lyon ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 ambayo italipwa baada ya kuruhusiwa kucheza.

Mshambuliaji huyo chipukizi wa Simba Wasiofungika, atalipwa Pauni Milioni 1.5 baada ya kusaini Mkataba wa miaka mitano na klabu ya White Hart Lane.
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino amelazimika kuongeza watu katika safu yake ya ushambuliaji ili kuiongezea makali kabla ya dirisha kufungwa Septemba 1, mwaka huu.

Na N'Jie anatarajiwa kuisaidia sana Spurs kutokana na umahiri wake katika safu ya ushambuliaji.

Kinda huyo aliyezaliwa Agosti 15, mwaka 1993 hadi sasa tayari ameichezea mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita. Alijiunga na Lyon mwaka 2010, baada ya kusukiwa mipango na kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo, Jean-Jacques Nono. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox