STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 31 Agosti 2015

MOURINHO AMGEUKIA HAZARD BAADA YA KIPIGO KUTOKA KWA PALACE


Jose Mourinho amesema kwamba, Eden Hazard lazima aongeze juhudi kurejesha kiwango chake baada ya kushuhudia mabingwa hao wa EPL wakifumuliwa magoli 2-1 nyumbani dhidi ya Crystal Palace wikendi iliyopita.

Magoli ya Bakary Sako na Joel Ward yaliipa pointi zote tatu Palace wakati Mourinho akisherehekea mchezo wake wa 100 akiwa nyumbani na kuwa kipigo cha pili tangu Mreno juyo akabidhiwe majukumu ya kukinoa kikosi hicho akiwa katika dimba la Stamford bridge.

Mourinho amemgeukia Hazard ambaye alishinda tuzo ya mchezaji bora wa msmu wa EPL msimu uliopita na wachezaji wengine baada ya timu hiyo kuwa na mwanzo mbovu wa ligi, wakiwa na pointi nne ambazo wamezipata katika michezo minne.  
"Kama wewe ni mchezaji bora katika ligi, nadhani itakuwa ni jambo jema kuwa na kiwango ambacho kinafanana na msimu uliopita”, alisema.

"Sitaki kuelezea kiwango cha mchezaji mmoja mmoja. Kwa ujumla, ni vigumu sana kuwa ni kiwango kile kile endapo baadhi ya wachezaji hawachezi vizuri.

"Ukiwa una wachezaji sita au saba wanacheza vizuri halafu watatu au wanne hawachezi vizuri, ni vigumu sana kupata matokeo".

Aliongeza kuwa anafanya kazi mchana na usiku kuhakikisha kuwa Chelsea inarejea katika ubora wake katika wiki zijazo, lakini amesema itakuwa ni huzuni kubwa endapo watabaki kuwa hivyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox