STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Ijumaa, 14 Agosti 2015

RASMI: AZAM TV KUONESHA LIVE LA LIGA, LEO WAZINDUA CHANNEL MPYA

KAMPUNI ya Azam Media leo imezindua rasmi chaneli yake mpya yenye ubora wa juu kabisa, iitwayo “Azam Sports HD”.Tangu kuanza kwa huduma za AzamTV, wateja wamekuwa wakijiuliza hasa ni kipi wanachopata kutokana na alama ya HD iliyo mbele ya kisimbuzi – kuanzia sasa watabaini. 

Baada ya miezi 18 ya mipango na uwekezaji, leo umeshuhudiwa uzinduzi wa chanel ya kwanza itakayowezesha wateja kufaidi picha na sauti zaubora wa juu kabisa “HD” kutokana na teknolojia ya kiwango cha juu. 

Wateja wa kifurushi chenye chaneli mpya ya “Azam Sports” wataweza kuona timu zao wazipendazo katika VPL katika picha ang’avu zaidi ambazo hazijawahi kuonekana. 

Zaidi, kampuni pia imetangaza rasmi ujio wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu La Liga ambayo wateja wataipata katika ubora wa HD kupitia Chanel mpya. Mchezo wa kwanza kuoneshwa katika msimu mpya wa La Liga 2015/16, ni Malaga dhidi ya  Seville wa Ijumaa Agosti 21, 2015 na timu zote vigogo zitakuwa zikicheza na kuoneshwa Live mwisho wa juma lijalo, na kila mzunguko wa msimu mzima katika ubora wa HD. 


Kifurushi kinachojumuisha chaneli ya Azam Sports HD kitaonekana kwa watazamaji wa AzamTV wa Tanzania pekee ambao wanalipia kifurushi chochote kati ya vitatu vya sasa; Pure, Plus au Play – na nyongeza ya ya SH15,000 kwa mwezi, ikijumuisha VAT. 

Pamoja na chaneli mpya ya Azam Sports HD, malipo hayo yatajumujisha chaneli za klabu za Manchester United, Liverpool na Real Madrid  ambazo kwa sasa ni sehemu ya kifurushi cha  Azam Play. 

Kadhalika malipo ya mwezi kwa kifurushi cha Play kitapunguzwa hadi Tsh25,000 kuanzia sasa. Kwa wale wasiokuwa na luninga zenye uwezo wa kuona picha za HD au waya maalum wa HD (HDMI), watapata chaneli mpya na kufuatilia La Liga na mengineyo – japo si kwa ubora wa HD.  

Pia kwa wateja wasiohitaji kujiunga na kiufurushi kipya hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kutoona michezo ya VPL kwani itaendelea kuoneshwa kupitia  Azam One na Azam Two kama ilivyokuwa kabla – Jambo lililo tofauti ni kuwa michezo yenye mvuto zaidi itaoneshwa pia kwenye Azam Sports HD.

Zaidi ya La Liga na VPL, Azam Sports HD itakuwa na vipindi mbalimbali vya kimichezo  vitakavyojumuisha michezo ya Ligi za soka za Uganda, Kenya na, Burundi – itakayoanza hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amesema “Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya AzamTV. 

Hata kabla ya ya kuanza mwaka 2013 tulijipanga kukidhi mahitaji ya teknolojia kwa ajili ya kutoa picha za ubora wa  HD ili kutuwezesha baadaye kumpatia mtazamaji picha bora zaidi bila kulazimika kununua vifaa vipya. 

Jambo ambalo hatukulitazamia ni kutekeleza hilo ndani ya muda mfupi – na kuanzisha chaneli  kwa kuonesha moja kwa moja soka la La Liga! Ambalo ni bora zaidi barani Ulaya. 

Uwezo wa kuona moja kwa moja na katika HD timu mzipendazo huko Hispania na kwa VPL, pamoja na vipindi vingine vya michezo kutoka sehemu mablimbali duniani, unatoa chaguo muhimu na ambalo wateja wetu wanalimudu. Huu ni mwanzo tu – jiandae kwa makubwa zaidi”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox