Hatma
ya Elius Maguri na Ivo Mapunda bado haijajulikana ndani ya klabu ya
Simba, huku kila mchezaji akiwa na mazingira tofauti ya ama kuendelea
kusalia kwenye klabu hiyo au kutokuwepo kabisa msimu ujao wa ligi kuu
Tanzania bara 2015-2016.
Rais
wa Simba SC, Evans Aveva ameweka wazi kuwa hatma ya Maguri iko mikononi
mwa kamati ya usajili ya klabu hiyo kufuatia kocha Dylan Kerr
kumuengua katika kikosi chake kilichocheza mechi ya Simba Day dhidi ya
SC Villa.
Kuhusiana na Ivo, Aveva amesema klabu yake inasubiri pande hizo mbili kukutana na kutiliana saini.
“Elius
Maguri jina lake halikuwepo kwa vigezo ambavyo mwalimu anavijua na sisi
kama wanasimba na ‘stake holders’ wa mpira, siku zote mmekuwa
mkiwapigia kelele viongozi hasa wa vilabu vya Simba na Yanga kwamba
tumekuwa tukiingilia majukumu ya walimu, sisi tukaona tuheshimu hilo
pamoja na kwamba Maguri tulimsajili kwa matumaini makubwa”, amesema
Evans Aveva
“Lakini
mwalimu alipokuja akaona uwezo wa Maguri ni mdogo kwa hiyo katika ile
mechi ya Villa akaona asishiriki, kinachofuata baada ya hapo ni
maongezi pamoja na viongozi wa Simba kujua hatma yake.
Zaidikuhusu Ivo, Aveva amefafanua kuwa, mazungumzo yameshafanyika na imebaki kutiliana.
“Ivo Mapunda ataendelea kuwa mchezaji wa Simba Sports Club katika kipindi kinachokuja”.
“Mazungumzo
yalifikia hitimisho na wakakubaliana, Ivo atakuja kusaini mkataba na
klabu yetu ya Simba, mpaka hivi ninavyozungumza ni kwamba ni bahati
usajili umesogezwa mbele, kwa hiyo bado tuna muda lakini mpaka hapa
ninavyozungumza Ivo bado hajaonekana kuja kusaini mkataba Simba, hivyo
jukumu hili limerudishwa tena katika kamati husika na Ivo bado yupo Dar
tutatoa majibu”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni