Kitabu kipya cha Kocha Sir Alex Ferguson kiitwacho Leading
kina mambo aisee.
Kocha huyo ametoa kitabu hicho akisimulia mambo mengi sana
wakati akiwa Kocha wa Manchester United na moja wapo ni wachezaji aliowahitaji
lakini akawakosa na baadaye wakawa nyota duniani kote.
Amanza na mshambuliaji Ronaldo de Lima wa Brazil ambaye
alimkosa, baadaye akatua PSV kabla ya kwenda Barcelona na baadaye akawa nyota
duniani kote.
Pia alimzungumzia nyota wa Bayern Munich, Thomas Muller ambaye
alimkosa akiwa na miaka 10.
Halafu akawataja nyota wawili wa Chelsea, baadaye. Je,
unawajua? Hao ni kipa Petr Cech pamoja na mshambuliaji hatari aliyestaafu,
Didier Drogba.
Anasema alimuona Drogba akiwa Marseille ya Ufaransa, klabu
hiyo ikataka pauni milioni 25. Wakati wanaulizana wafanyeje, Chelsea
wakawawahi.
Kwa upande wa Ronaldo, naye alikuwa tayari kujiunga wakati
akicheza kwao, lakini suala la kibali cha kazi likawa tatizo, mwisho akaenda
zake PSV.
Mwingine ni Sergio Aguero ambaye hadi makubaliano yalianza,
lakini alilalama kwamba wakala wake alitibua kwa kutaja bei kubwa sana.
Wakashindwa.
Lucas Moura, pia Ferguson akamtaka na wakawa tayari kutoa
pauni milioni 24, lakini mamilionea wa Ufaransa, PSG wakaibuka na kuweka mezani
pauni milioni 45.
Beki Raphael Varane ambaye sasa anakipiga Real Madrid pia
alikuwa chaguo lake, wakakubaliana na mwisho Zinedine Zidane akaingilia na
kumpeleka Madrid.
“Ilikuwa ni Zidane, nakumbuka wakati huo Mourinho ndiye
alikuwa kocha wa Real Madrid. Lakini sidhani kama hata aliwahi kumuona akicheza
hadi alipopelekwa na Zidane,” alisema.
WENGINE:
Ferguson aliwataja wachezaji wengine aliowahi kutaka
kuwasajili lakini akawakosa kuwa ni washambuliaji hatari enzi hizo kama Alan
Shearer pia Patrick Kluivert.
Kwa sababu tofauti, aliwakosa Gabriel Omar Batistuta, Samir Nasri na Glenn
Hysen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni