Ligi kuu ya Uingereza Barclays Premier League imeendelea tena jumamosi ya leo tarehe 29, September – mchezo wa kwanza siku ya leo umewakutanisha Manchester City dhidi ya Tottenham Hotspur.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la White Hart Lane umemalizika kwa City kupata kipigo kizito kutoka kwa Spurs.
Spurs walianza kuliona lango la Spurs katika dakika ya 25 kwa goli lilofungwa na mchezaji mpya City De Bruyne – Spurs wakafanikiwa kusawazisha dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza, goli likifungwa na beki wa pembeni Eric Dier.
Dakika 5 baada ya mapumziko Spurs wakapata goli la pili lilofungwa na beki wa kati Alderweireld na muda mfupi baadae mfungaji bora wa Spurs msimu uliopita Harry Kane akafungua akaunti yake ya magoli msimu huu kwa kufunga goli la 3.
Dakika ya 79 Winga wa kiargentina Eric Lamela akashindilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la City kwa kufunga goli la nne.
TIMU ZILIPANGWA HIVI
Tottenham (4-2-3-1): Lloris 7.5, Walker 6, Alderweireld 7, Vertonghen 7, Davies 6, Dier 8, Alli 6, Lamela 7 (Carroll 87), Son Heung-min 6 (N’Jie 75), Eriksen 6.5 (Chadli 68), Kane 7
Subs not used: Rose, Vorm, Trippier, Townsend, Carroll
Booked: Lamela, Dier, Eriksen, Alli, Kane
Scorers: De Bruyne 25
Manchester City (4-5-1): Caballero 4.5, Sagna 6, Demichelis 5, Otamendi 5.5, Kolarov 5, Fernandinho 6 (Nasri 69), Fernando 6, De Bruyne 6.5, Toure 5.5 (Jesús Navas 56), Sterling 5, Aguero 5 (Roberts 86)
Subs not used: Hart, Zabaleta, Barker, Evans
Booked: Demichelis
Scorers: Dier 45, Alderweireld 50, Kane 61, Lamela 79
Referee: Mark Clattenburg 4.5
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni