STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 19 Septemba 2015

MATOKEO YA MICHEZO YA LEO LIGI KUU TANZANIA BARA, YANGA WATOA DOZI, MAJIMAJI YAFIA TANGA





Mabingwa wa ligi kuu ya vodacom yanga sc wameendeleza wimbi lao la ushindi katika mchezo wake wa tatu wa ligi kuu ya vodacom baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 4-1 mbele ya JKT Ruvu mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.


Katika mchezo huo wa leo ambao ulianza kwa kasi ya chini huku timu zote zikicheza mpira wa chini Yanga ndio walikuwa wa mwanzo kufika katika lango la JKT Ruvu katika dakika ya 1 ya mchezo ambapo Donald Ngoma akiwa na kipa alipiga shuti lililo gonga mwamba.

JKT Ruvu wakicheza soka la kujiami na kujikuta muda mwingi wakikwa katika eneo lao na kupelekea yanga kuchelewa kupata goli la kwanza na wakishindwa kutengeneza nafasi za wazi za kutosha.


Iliwachukuwa dakika ya 33 Yanga kufanikiwa kupenya ngome ya JKT Ruvu na kufanikiwa kupata goli kupitia kwa Donald Ngoma, baada ya kugongeana na Amisi Tambwe, na kuipeleka yanga mapumziko wakiwa mbele kwa goli 1-0.


Katika kipindi cha pili Yanga SC walikuja kwa kasi kwa dhumuni ya kumaliza mchezo mapema ambapo dhamira yao ilitimia katika dakika ya 47 baada ya Amisi Tambwe kuunga krosi ya Deusi Kaseke na kupia yanga goli la pili.


Kuingia kwa goli hilo kulipelekea JKT Ruvu kufunguka na kuanza kusaka goli ambapo katika dakika ya 50 walifanikiwa kupata goli kupitia kwa Michael Aidan, akiunga mpira wa adhabu ulio wagonga mabeki wa yanga sc.


Kuingia kwa goli hilo kulizidisha kasi ya yanga wakiwa katika eneo la JKT Ruvu ambapo katika dakika ya 62 Amisi Tambwe aliifungia yanga goli la 3 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa JKT Ruvu Tomy Kavishe.


Muhutimishaji wa magoli ya yanga leo alikuwa kiungo Thaban Kamusoko ambap[o katika dakika ya 86 alipiga shuti nnje kidogo ya eneo la hatari na kutinga moja kwa mjoa katika nyavu za JKT Ruvu na kuipa ushindi yanga wa magoli 4-1.


Kwa matokeo hayo yanaifanya yanga kufikisha pointi 9 baada ya kucheza michezo mitatu na kujikita kileleni mwa ligi kuu ya vodacom.


Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thabani Kamusoko, Simon Msuva, Haruna Niyonzima/Salum Telela dk78, Amksi tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Godfrey Mwashiuya dk61.


JKT Ruvu; Tony Kavishe, Michael Aidan, Napho Zuberi, Martin Kazila, Ramadhani Madenge, George Minja, Ismail Aziz/Abdulrahman Mussa dk57, Nashon Naftali, Samule Kamuntu/Gaudence Mwaikimba dk57, Saad Kipanga/Emmanuel Pius dk77 na Mussa Juma. 


MATOKEO MECHI ZA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA LEOStand United 2-0 African Sports Mgambo Shooting 1-0 Majimaji FCPrisons 1-0 Mbeya CityYanga SC 4-1 JKT Ruvu


Kesho Septemba 20, 2015Mwadui FC Vs Azam FCMtibwa Sugar Vs Ndanda FCSimba SC Vs Kagera SugarCoastal Union Vs Toto Africans


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox