STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 29 Oktoba 2015

AZAM FC YAPAA KILELENI LIGI KUU...........


Didier Kavumbangu (kushoto) akishangilia na Farid Mussa baada ya kufunga bao la kwanza leo


AZAM FC imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-2 jioni ya leo Uwanja wa Karume, Dar
 
Ushindi huo unaifanya timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi nane, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi, Yanga SC ambao jana walilazimishwa sare ya 2-2 na Mwadui mjini Shinyanga.
 
Kwa ushindi wa leo, sifa zimuendee mshambuliaji Mrundi, Didier Kavumbangu ambaye amefunga bao moja na kuseti mengine mawili, moja la John Bocco na lingine la Kipre Tchetche. 
 
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo, hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
 
Mrundi Didier Kavumbangu alianza kufunga bao la kwanza dakika ya tano kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya kiungo wa Ivory Coast, Kipre Michael Balou.
Kavumbangu tena akamsetia Bocco krosi nzuri kufunga bao la pili dakika ya saba, kabla ya Najim Magulu kuifungia JKT Ruvu dakika ya 31.
 
JKT walicharuka baada ya kupata bao na kupeleka mashambulizi ya nguvu langoni mwa Azam FC, lakini hawakuwa na bahati ya kufunga.
 
Kipindi cha pili, Azam FC ilikianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 64, mfungaji Bocco kwa penalti baada ya beki wa JKT Ruvu, George Minja kumkwatua beki wa Azam FC, Shomary Kapombe.
 
Kabla Azam FC hawajamaliza kushangilia bao lao la tatu, JKT Ruvu wakapata bao la pili dakika ya 69 kupitia kwa Emmanuel Pius aliyetumia makosa ya mabeki wa Azam FC kuchanganyana.
 
Wakati JKT wapo kwenye jitihada za kusaka bao la kusawazisha, Azam FC walifanikiwa kupata bao la nne lililofungwa na Kipre Herman Tchetche aliyepokea pasi ya Kavumbangu.    
 
Kikosi cha JKT Ruvu kilikuwa; Shaaban Dihile, Michael Aidan, Paul Mhidze, Renatus Morris, George Minja, Hamisi Shengo, Mussa Juma, Issa Ngao, Gaudence Mwaikimba/Samuel Kamuntu dk46, Najim Magulu/Abdulrahim Mussa dk73 na Saady Kipanga/Emmanuel Pius dk60.
 
Azam FC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Said Mourad, Aggrey Morris, Serge Wawa, Kipre Bolou/Himid Mao dk46, Salum Abubakar `Sure Boy`, Jean Mugiraneza `Migi`, John Bocco `Adebayor`/Kipre Tchetche dk77, Didier Kavumbangu na Farid Mussa/Erasto Nyoni dk70.
 
 MATOKEO YA LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA
 
Oktoba 29, 2015

Prisons 1-0 African Sports
JKT Ruvu  2-4 Azam FC 
 
Oktoba 28, 2015
Toto African 1-0 Mgambo Shooting
Mwadui FC 2-2 Yanga SC
Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar
Mbeya City 1-1 Majimaji FC
Ndanda FC 0-0 Stand United
Simba Sc 1-0 Coastal Union
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox