Mataifa mawili yanayojulikana sana
kwa kusakata gozi Amerika Kusini yalicharazwa kwenye mechi za kufuzu
kwa Kombe la Dunia zilizochezwa Alhamisi.
Mambo hayakuwa sawa kwa Argentina waliokubali kichapo cha 2-0 nyumbani kutoka kwa Ecuador, wakicheza bila nyota wao wa Barcelona Lionel Messi.
Chile walishinda kupitia mabao mawili ya kipindi cha pili kutoka kwa Eduardo Vargas na Alexis Sanchez.
Neymar anatumikia kifungo cha mechi mbili za mwisho kati ya nne alizosimamishwa kucheza miezi mitatu iliyopita wakati wa Copa America. Pia atakosa mechi ya wiki ijayo dhidi ya Venezuela.
Mjini Buenos Aires, miamba wa soka Argentina, walikubali kupokea mabao mawili kipindi cha pili kutoka kwa Frickson Erazo na Felipe Caicedo wa Ecuador.
Nyota wao Messi anauguza jeraha la goti na anatarajiwa kurejea uwanjani mwishoni mwa Novemba.
Argentina hata hivyo walikuwa na nyota wengi uwanjani, wakiwemo Angel Di Maria, Sergio Aguero and Javier Macherano.
Kweye mechi nyingine za kufuzu Alhamisi, Uruguay walilaza Bolivia 2-0 mjini La Paz kupitia Martin Caceres na Diego Godin.
Uruguay walishinda bila Luis Suarez na Edinson Cavani.
Paraguay nao walilaza Venezuela 1-0, bao hilo pekee la mechi hiyo likitoka kwa Derlis Gonzalez dakika ya 84.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni