Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL)
inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja
mbalimbali nchini, ikiwa katika mzunguko wa saba timu 14 zitapambana kusaka
pointi 3 muhimu.
Young Africans watawakaribisha Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, huku timu zote zikiwa na pointi 15 kileleni zikitofautiana kwa magoli ya kufunga na kufungwa.
Kabla ya mchezo wa Yanga dhidi ya Azam,
kutakua na mchezo wa utangulizi wa kuombea amani kuelekea kwenye uchaguzi mkuu
wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 25, 2015.
Mchezo huo utawakutanisha viongozi wa
dini watakocheza dhidi ya mabalozi wanaofanya kazi nchini, mechi hiyo itaanza
saa 8:25 mchana na kumalizika saa 9:15 alasiri.
Majimaji FC ya mkoani Ruvuma watakua
wenyeji wa African Sports kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea, huku Ndanda
FC wakiwakaribisha Toto African kutoka jijini Mwanza katika uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara.
Jijini Mbeya, watoza ushuru wa jijini
hilo Mbeya City FC watawakaribisha Simba SC katika uwanja wa Sokoine, Chama la
wana Stand United watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons uwanja wa Kambarage
mjini Shinyanga, huku Coastal Union wagosi wa kaya wakiwakaribisha wakata miwa
wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo itaendelea Jumapili kwa
michezo miwili kuchezwa, Mgambo Shooting watakua wenyeji wa Kagera Sugar katika
uwanja wa Mkwakwani, huku Mwadui FC wakicheza na maafande wa JKT Ruvu katika
uwanja wa Mwadui Complex.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni