STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 29 Oktoba 2015

KIMENUKA,CAF YACHARUKA YATAKA ZFA IACHANE NA KUPELEKA MAMBO YA SOKA MAHAKAMANI

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo hii limeamuru Kamati ya muda inayoongoza Chama cha Mpira Zanzibar (ZFA) iondoe mahakamani mashatka yote dhidi ya uongozi halali wa ZFA.
Katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa ZFA na nakala yake kuletwa TFF, CAF imesisitiza kuwa kwa mujibu wa katiba za CAF na FIFA ni marufuku masuala ya mpira kupelekwa mahakamani, ZFA ni mwanachama mshiriki wa CAF (Associate Member).
CAF inaigiza kamati ya muda ya ZFA hadi tarehe 07 Novemba, 2015 iwe imetekeleza maagizo na kuhakikisha uongozi halali uliochaguliwa na ZFA unarejea katika shughuli zake uongozi ZFA.
Jambo hili lisipotekelezwa CAF imesema itaifungia Zanzibar uanachama wake. Kikanuni na kikatiba kufungiwa uanachama maana yake ni Mwanachama husika kusitishwa ushiriki katika shughuli zote zinazosimamiwa na FIFA, CAF na wanachama wake wote.
Shughuli hizo ni pamoja na kushiriki mashindano ya kimataifa, kozi mbalimbali na misaada ya kifedha, vifaa, ufundi nk.
TFF inatoa wito kwa mara nyingine kwa pande zinazokinzana kukaa meza moja na kumaliza tofauti zao kwa faida ya mpira wa Zanzibar, Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox