MENEJA wa Liverpool,
Brendan Rodgers amesema haofii chochote kuhusu kibarua chake kufuatia
kuanza kwa kusuasua msimu huu.
Liverpool imefanikiwa kupata ushindi
katika mchezo mmoja kati ya mitano ya Ligi Kuu huku wakielekea katika
mchezo mwingine mgumu dhidi ya mahasimu wao wa jiji Everton Jumapili
hii.
Liverpool inashika nafasi ya tisa katika msimamo wa ligi nafasi nne
na alama moja nyuma ya Everton.
Akihojiwa Rodgers amesema siku zote
amekuwa akifanya kazi nzuri kadri awezavyo hivyo haofii chochote katika
nafasi hiyo.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa anachozingatia ni
kuangali jinsi watakavyopata alama tatu muhimu katika mchezo huo dhidi
ya mahasimu wao ambao utafanyika katika Uwanja wa Goodison Park.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni