pichaz
za wale wakali wetu wa michezo ambao tumewazoea kuwaona wakiwa na timu
zao pamoja na mafanikio yao ila huku ndipo walipotokea mastaa hawa.
1- Lewis Hamilton kama ni mpenzi wa mbio za magari ya Formula One basi jina lake sio geni akilini mwako, mkali huyu aliyezaliwa January 7 1985 Stevenage Uingereza
amewahi kushinda medali kadhaa katika mbio za magari. Staa huyu kama
ulikuwa hujui amelelewa na mama kwa kiasi kikubwa toka akiwa na umri wa
miaka miwili hii ilitokana na baba yake na mama yake kutengana.
2- Eden Hazard ni raia na mchezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji pamoja na klabu ya Chelsea, kuna usemi unasema maji ufuata mkondo Eden Hazard kazaliwa katika familia ya wachezaji soka, mama yake mzazi Carine alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Ubelgiji na baba yake Thierry alikuwa mchezaji soka katika nafasi ya kiungo mshambuliaji, hivyo usishangae kumuona Hazard akionyesha umahiri mkubwa uwanjani.
3- Robert Lewandowski kuna
wakati alikuwa akitajwa kama ni moja kati ya washambuliaji hatari
zaidi, haishangazi kumuona akicheza soka kwani ametokea katika familia
ya wanamichezo, baba yake Krzysztof alifariki mwaka 1995 lakini pia aliwahi kuwa bingwa wa mchezo wa Judo nchini kwao Poland. Mama yake mzazi Iwona alikuwa mchezaji wa volleyball.
4- John Terry ni beki wa kati wa klabu ya Chelsea na nahodha wa klabu hiyo amecheza timu ya taifa ya Uingereza kwa muda mrefu, ametoka mbali katika soka kwani alianza kucheza soka katika timu ya Senrab kabla ya mwaka 1991 kuhamia katika timu ya vijana ya West Ham United hapo ndio ulikuwa mwanzo wa mkali huyo wa soka.
5- Neymar da Silva Santos hata kama sio mpenda soka sana lazima utakuwa umewahi kulisikia jina lake, kwa sasa anacheza klabu ya FC Barcelona ya Hispania. Neymar hakuanza kucheza soka moja kwa moja katika Academy za soka, alianzia mtaani kucheza soka. Jina lake Neymar da Silva Santos Junior amerithi kwa baba yake ambaye alikuwa mchezaji soka hivyo Neymar amerithi kipaji kutoka kwa baba yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni