STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 31 Desemba 2015

HII INAKUHUSU WEWE MDAU WA BLOG NA MSIKILIZAJI WA PLANET SPORTS

www.asantemuya.blogspot.com inachukua nafasi hii kukutakia heri ya mwaka mpya wewe mdau wetu ambae umekuwa pamoja nasi tangu kuanzishwa kwa ukurasa huu ambao umekuwa unakujuza habari za michezo kitaifa na kimataifa bila kusahau na makala mbalimbali za kimichezo.

Waendeshaji wa blog hii (Hemed Muya pamoja na Mr'Choi)  sote kwa pamoja tunaimani mwaka 2016 wewe mdau wetu tutazidi kuwa pamoja kama mwaka 2015 lakini pia kwa upande wetu yapo mengi ambayo tumepanga kuwaletea wasomaji wetu.

Lakini pia kama ambavyo tunafahamu blog hii inaendeshwa na watangazaji wa kituo cha radio kilichopo mkoani Morogoro "Planet fm-87.9" hivyo pia kwa wale wasikilizaji wetu wa mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani vilevile wale wanaotufuatilia online "www.planetfmtz.com" tunapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana kwa maana bila sapoti yako tusinge fika hapa tulipo fika.

Katika kazi changamoto zipo nyingi sana na kwakuwa mmeshatujuza sehemu za kufanya marekebisho katika blog na kipindi chetu cha michezo ''Planet sports'' ambacho hukujia majira ya saa mbili usiku kila siku tunapenda kuwajuza maoni yenu tutayafanyia kazi na mabadiliko mtayaona.

Pia nachukua nafasi hii kuwajuza wasikilizaji wetu kwamba kipindi cha michezo kitakuwa na masaa mawili kwa siku na hii inatokana na maoni ya wengi kuwa kipindi kiongezewe muda ilituweze kuwafahamisha mengi ya kimichezo ratiba kamili hii hapa chini.

      RATIBA YA VIPINDI VYA MICHEZO PLANET FM-87.9

 HOT ON SPORTS- JUMATATU-IJUMAA SAA 10:00 MPAKA 11:00 ASUBUHI.
                                   -Hot News
                                   -Penalt Box
                                   -Face to face
                                  -Transfer zone

 PLANET SPORTS- JUMATATU-JUMAPILI SAA 20:00 MPAKA 21:00 USIKU.

-Habari za siku michezoni Kitaifa,Kimataifa,Uchambuzi yakinifu na Sports details.



 PLANET WEEKLY SPORTS- JUMAPILI SAA 13:00-15:00 MCHANA.

               -Matukio makubwa yaliojiri michezoni kwa wiki nzima yatachambuliwa kwa kina yote ya kitaifa na kimataifa.

Kupitia vipindi hivyo vya kimichezo msikilizaji wetu utayapata  mengi ya kimichezo na uchambuzi yakinifu uliobobea kutoka kwa wachambuzi bora kabisa Mr'Choi,Adam Kassimu na Salum Mapande hivyo usikose kusikiliza uhondo huo wa kimichezo ukiongozwa na mimi Hemed Muya.

Najua wengi mnafahamu timu nzima ya kipindi cha michezo imebobea katika habari za hapa nyumbani pamoja na kimataifa na moja kati ya wachambuzi wetu Mr'Choi alizungumza hiki.

"Binafsi nawashukuru sana wasikilizaji wetu ambao wamekuwa pamoja nasi kwa amahakika wameshuhudia utofauti wenye ubora kwa kiasi kikubwa sana tangu muunganiko wa sasa wa timu ya michezo kuwepo.

  Leo hii tunajeuri ya kusema sisi ni bora kuliko vipindi vyote vya michezo Tanzania  nnje ya radio za Dar es Salaam ambazo na zenyewe tumezidiana katika baadhi ya sehemu hasa habari za hapa nyumbani na ni swala ambalo tunashuhulikia ili mwisho wa siku na wao tuwakalishe.

 Ninacho wajuza wasikilizaji wetu kuwa mwaka 2016 ni mwaka wa Mchaka-mchaka hivyo wataraji mazuri ya kimataifa na kitaifa katika kila engo kama kawaida yangu.

 Namalizia kwa kusema wategemee uchambuzi uliobobea pia wajiandae kwa makala zangu kupitia blogg hii bila kusahau Sports Details katika ubora wangu tuombeane na tuwe kitu kimoja.'' Mr Choi

Hayo ni baadhi aliosema Choi lakini pia wachambuzi wote na mimi Muya tunapenda kuwajuza mkae mkao wa kula kusikiliza vipindi vya kimichezo na kutembelea  blog hii  bila kusahau ukurasa "page'' ya facebook Asante Muya na Mbwembwe Dimbani.

  Sote kwa pamoja kwa kudra za mwenyezi Mungu atujalie uzima na tuwe pamoja.

                          HAPPY NEW YEAR-2016 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox