STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 31 Desemba 2015

ROONEY, JOE HART, CAHILL, STERLING, KANE KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA ENGLAND, WENGINE WAPO HAPA

ENGLAND imeanika Listi ya Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yao ambapo pia ipo Tuzo kwa Chipukizi Vijana wa chini wa Miaka 21, U-21.

Kepteni wa England, Wayne Rooney, ambae alishinda Tuzo hiyo Mwaka Jana, ni miongoni mwa Wachezaji Watano wanaogombea. 


Rooney Mwaka huu aliiongoza England kufuzu kuingia Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, ambazo zitachezwa huko France Mwezi Juni huku akihakikisha England inashinda Mechi zao zote 10 za Kundi lao.

Pia, Mwaka huu, Rooney aliivunja Rekodi ya Sir Bobby Charlton ya Ufungaji Bora katika Historia ya England kwa kufunga Bao 50 Rekodi ambayo iliwekwa na Charlton Mwaka 1968 alipofunga Bao lake la 49. 

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka:

Joe Hart (Manchester City)
Gary Cahill (Chelsea)
Raheem Sterling (Manchester City)
Wayne Rooney (Manchester United)
Harry Kane (Tottenham Hotspur)

Kwa Vijana wa U-21, Straika wa Man United, Jesse Lingard, yumo kwenye Listi ya Wagombea Watano na huenda akashinda baada ya kung’’aa alipoichezea England U-21 Mwezi Juni Mwaka huu huko Czech Republic kwenye Fainali za Ulaya za U-21.

Wagombea Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa U-21:

Jack Butland (Stoke City)
Carl Jenkinson (West Ham United)
James Ward-Prowse (Southampton)
Jesse Lingard (Manchester United)
Nathan Redmond (Norwich City) 


Kura kwa Wagombea zitapigwa mtandaoni na Masapota wa England na upigaji utafungwa Jumapili Januari 3.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox