KOCHA Louis van Gaal ametoa hotuba yenye hisia kali jana kwa wachezaji Manchester United na viongozi katika jithada za kuokoa kibarua chake akisema wanapaswa kushikamana katika kipindi hiki kigumu.
Kocha
huyo wa United alipigiwa makofi na karibu watu 200 wakati sherehe ya
Krisimasi makao makuu ya klabu, viwanja vya Carrington iliyokwenda
sambamba na chakula cha mchana.
"Sisi
ni Manchester United na tutakuwepo — lakini lazima tushikamane," huo
ndiyo ulikuwa ujumbe wa Van Gaal ingawa utamaduni wa asili wa mechi ya
timu za vijana za United uliahirishwa.
Kocha Louis van Gaal ametoa hotuba yenye hisia kali jana wakati wa sherehe za Krisimasi Manchester United jana mchana
Van
Gaal anakabiliwa na shinikizo baada ya kucheza mechi tatu mfululizo
bila ushindi, mara ya mwisho Jumamosi akifungwa 2-1 nyumbani na Norwich
City.
Wamiliki
wa United, Wamarekani familia ya Glazer, na Mwenyekiti, Ed Woodward
inafahamika wanafikiria kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na
wamefanya mawasiliano na wawakilishi wa kocha Mreno, Jose Mourinho,
ambaye alifukuzwa Chelsea wiki iliyopita.
Mourinho tayari ameweka wazi kwamba yuko tayari kurejea kazini haraka.
Vyanzo
vya habari ndani ya United vinasema kwamba klabu hiyo inafanya mpango
wa kumshawishi Mourinho kupitia wakala wake, Jorge Mendes ili atue Old
Trafford.
Mendes
ni mtu aliyefanya kazi kwa karibu na kocha Sir Alex Ferguson na
Mtendaji Mkuu wa zamani, David Gill aliyewasaidia kuwapata nyota kama
Cristiano Ronaldo, Nani, Anderson, Bebe na David de Gea wakatua United.
Siku
za karibuni amekuwa akifanya kazi na Woodward pia na ndiye
aliyefanikisha mipango ya kusajiliwa kwa Radamel Falcao na Angel di
Maria, pamoja na De Gea kukubali kusaini Mkataba mpya.
Pamoja na hayo, Van Gaal anataka kutumia fursa hii kurudisha matokeo mazuri ndani ya klabu wakati wa Krisimasi akikabiliwa na mechi ngumu dhidi ya Stoke City na Chelsea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni