Mchezo kati ya Azam vs Mtibwa Sugar umemalizika kwa timu hizo kutoka
sare ya kufungana kwa goli 1-1 kwenye mchezo wa pili wa Mapinduzi Cup
ulionza majira ya saa 2:15 usiku na timu hizo kugawana pointi mojamoja.
Mtibwa Sugar waliandika goli lao dakika ya 61 kipindi cha pili
kupitia kwa mshambuliaji wao Hussein Javu aliyerejea kwenye timu yake ya
zamani mara baada ya kutemwa na kikosi cha Yanga. Javu alifunga goli
hilo akimalizia pasi ya Kichuya ambaye aliunasa mpira kutokana na makosa
ya mlinzi wa Azam FC Said Mourad.
Dakika ya 74 nahodha wa Azam FC John Bocco ‘Adebayor’ aliisawazishia
timu yake kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi
kwenye eneo la hatari la Mtibwa Sugar.
Kama kawaida inapopigwa mechi kati ya Azam FC vs Mtibwa Sugar huwa ni
zaidi ya fainali, timu hizi zimekuwa na upinzani mkubwa sana. Kabla ya
kukutana kwenye mchezo wa leo timu hizi zilikutana kwenye mchezo wa ligi
kuu Tanzania bara uliopigwa Jumatano iliyopita kwenye uwanja wa Azam
Complex na Azam kupata ushindi wa goli 1-0 na kufanikiwa kuongoza ligi.
Kwenye mchezo wa leo, Mtibwa waliwashika vilivyo Azam na kuwaweka
‘mfukoni’ huku wakisukuma mpira wa haraka na kuliweka lango la Azam
kwenye presha kwa muda wote wa kipindi cha kwanza na kipindi cha pili.
Unaweza ukasema Mtibwa wamekuwa hawawezi kucheza na nafasi kutokana na
kupoteza nafasi ambazo wamekuwa wakizitengeneza.
Wakati mchezo huo ukielekea ukingoni, Mtibwa walipata bao la pili
lakini mwamuzi wa mchezo alilikataa kwa madai kwamba mfungaji alikuwa
ameotea. Kukataliwa kwa goli hilo kulizua ‘mtiti’ kwa mshika kibendera
ambaye ndiye alinyoosha kibendera kuashiria mfungaji aliotea.
Lakini baada ya kumalizika kwa mchezo ilibidi waamuzi watolewe kwa
msaada wa ulinzi mkali wa polisi kutokana na wachezaji na benchi zima la
ufundi la Mtibwa Sugar kuwazonga waamuzi hao.
TANGAZA NASI: +255 655 442 255
CHANZI OPEN SCHOOL
Jumapili, 3 Januari 2016
Home
/
Unlabelled
/
AZAM YAPONEA KATIKA TUNDU LA SINDANO MBELE YA MTIBWA SUGAR HUKU WAAMUZI WAKINUSURIKA KUCHEZEA KICHAPO..........
AZAM YAPONEA KATIKA TUNDU LA SINDANO MBELE YA MTIBWA SUGAR HUKU WAAMUZI WAKINUSURIKA KUCHEZEA KICHAPO..........
About asantemuya
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni