STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 4 Januari 2016

LICHA YA KUTANGAZA KUACHANA NAYE, YANGA YATUMA JINA LA NIYONZIMA CAF

 


































Haruna Niyonzima ni miongoni mwa majina 24 ya wachezaji wa Yanga SC yaliyotumwa Shirikisho la Soka Africa (CAF) kwa ajili ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pamoja na Yanga SC kutangaza kuvunja Mkataba na Haruna – lakini hakuna hatua zaidi ilizochukua kuashiria kwamba huo ni uamuzi wa dhati, ikiwemo kumpa barua mchezaji mwenyewe kumfahamisha juu ya uamuzi huo.

Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halijapewa taarifa yoyote ya maandishi na Yanga SC juu ya uamuzi wa kuvunja Mkataba na Haruna.
Majina yaliyotumwa na Yanga SC CAF ni makipa; Ally Mustapha ‘Barthez’, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Benedict Tinocco.

Mabeki; Nadir Haroub ‘Cannavaro, Kevin Yondan, Mwinyi Hajji, Pato Ngonyani, Vincent Bossou, Juma Abdul, Mbuyu Twite na Oscar Joshua, wakati viungo ni Haruna Niyonzima, Thabani Kamusoko, Said Juma, Salum Telela.
 
Washambuliaji ni Donald Ngoma, Amissi Tambwe, Simon Msuva, Godfrey Mwashiuya, Paul Nonga, Malimi Busungu, Issoufou Boubakar, Matheo Anthony na Deus Kaseke.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox