STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatatu, 11 Januari 2016

KICHEKO KWA SIMBA FIFA YATOA SIKU 60 WAWE WAMEINGIZIWA MKWANJA WAO...............

 Tokeo la picha la SIMBA FC

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) iliyokutana Disemba 15 mwaka jana, imeiagiza klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuilipa Simba SC ya Tanzania pesa za uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi ndani ya siku sitini (60) kuanzia Januari 7, 2016.
  Katika taarifa hiyo ya FIFA na nakala yake kutumwa kwa TFF, Etoile du Sahel na Simba SC, Kamati ya Nidhamu imefikia uamuzi huo baada ya klabu ya Etoile du Sahel kupuuza kuilipa klabu ya Simba SC kiasi cha dola za kimarekani 300,000 za uhamisho wa mchezaji wa Emmanuel Okwi uliofayika Januari 2014.
Emmanuel Okwi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe

Katika barua hiyo ya maamuzi ya kikao hicho, Kamati ya Nidhamu imesema baada ya siku sitini (60) zilizotolewa kwa klabu ya Etoile kuwa imeilipa Simba SC kumalizika bila malipo hayo kuwa yamaefanyika, wataagiza Etoile du Sahel kukatwa pointi sita katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Tunisia.
  Na kama klabu ya Etoile itashindwa kulipa deni hilo hata baada ya kukatwa pointi sita, Kamati ya Nidhamu ya FIFA itaamua kuishusha daraja klabu hiyo kutoka Ligi Kuu mpaka ligi daraja la kwanza.
  Chama cha Soka nchini Tunisia (FTF) kimekumbushwa kutekeleza maelekezo hayo ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ya kuipokonya pointi sita Etoile du Sahel, na endapo FTF itashindwa kufanya hivyo basi itafungiwa kujishugulisha na shughuli zote za mpira zinazosimamiwa na FIFA.
  Aidha Kamati ya Nidhamu ya FIFA pia imeigiza klabu ya Etoile du Sahel kulipa faini ya dola za kimarekani 20,000 ndani ya siku sitini (60) baada ya kupokea uamuzi huo wa kamati.
  TFF imepewa jukumu la kuhakikisha Simba inalipwa deni hilo ndani ya muda uliopangwa wa siku sitini (60) na endapo klabu ya Etoile du Sahel itashindawa kufanya hivyo basi TFF iitarifu kamati ya nidhamu ya FIFA juu ya suala hilo.
  Kikao hicho cha Kamati ya Nidhamu kiliiongozwa na Mwenyekiti Claudio Sulser (Uswisi), Makamu Mwenyekiti Kia Tong Lim (Singapore), na mjumbe Fiti Sunia (Visiwa vya Samoa).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox