Droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la Fa imetoka huku timu za ligi kuu ya England zikipangwa na zile za daraja la chini.
Man City wao watakipiga na mshindi wa mchezo wa Wycombe Wanderers au Aston Villa. Huku majirani zao Man United wao watakipiga na Derby County.
West Ham, wanasubiri mshindi wa mchezo unaowakutanisha Exeter City dhidi ya majogoo wa Anfield Liverpool.\
Michezo hii ya raundi ya nne itachezwa January 29 mpaka Februari 1.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni