STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 6 Januari 2016

RATIBA YA RAUNDI YA TATU KOMBE LA SHIRIKISHO IKO HAPA, BURKINA FASO USO KWA USO NA SIMBA, YANGA WAPEWA FRIENDS RANGERS

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhUO-8i6dPmne5d1EhMMF6BmYFADMH1byPwHA9cHmyRVZcndUMHFapEuY1gN3j6l3RVMlMwpWtvkKxMpCm6PqnVhywypnk19c1r5HByhP6b6x7CNk_Xc9eLYlhPnFPHv0JEu-VS3Pti68Q/s320/Screenshot_2015-09-11-11-13-05-1.png

Baada ya kumalizika kwa raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho, ratiba ya hatua inayofauta ya michuano hiyo imetoka.

Vigogo wa Ligi Kuu, Simba, Azam na Yanga wamepangiwa timu za Ligi Daraja la Kwanza huku mechi mbili zikipambanisha timu za Ligi Kuu pekee.

Simba wao wamepangiwa kusafiri kucheza ugenini dhidi ya timu ya ligi Daraja la Kwanza, Burkina Faso ya Morogoro tarehe 23 mwezi huu.

Mabingwa wa Ligi Kuu, Yanga watapambana na klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Friends Rangers ya jijini Dar kwenye uwanja wa Taifa. Azam watakuwa wageni wa African Lyon kwenye dimba la Karume.

Mahasimu wa Shinyanga, Stand United na Mwadui wataoneshana ubabe kwa mara nyingine kwenye uwanja wa Kambarage. 

Pia mahasimu wa Tanga, African Sports na Coastal Union watatoana jasho wenyewe kwa wenyewe katika raundi ya tatu.

Mechi za raundi ya tatu zitachezwa kati ya Januari 23 na Februari 2. Bingwa wa kombe la Shirikisho atabeba kitita cha TSh milioni 50 pamoja na kuiwakilisha Tanzania Bara kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Ratiba kamili:
Majimaji v JKT Mlale
Pamba   V   Toto Africans
Burkina Faso   V   Simba
Ndanda   V    Mshikamano
Yanga   V  Friends Rangers
Njombe   V   Prisons
Stand United  V   Mwadui
Kagera Sugar  V  Rhino Rangers
Panone  V  Madini
Mtibwa Sugar   V  Abajalo
Lipuli/ Kurugenzi  V  JKT Ruvu
African Lyon  V  Azam
African Sports  V  Coastal Union
Geita Gold  V  Mvuvumwa
Singida  V  Mgambo
Wenda  V  Mbeya City

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox