STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumapili, 3 Januari 2016

YANGA WANG'ARA ZANZIBAR,NGOMA AFANYA YAKE..........

 Tokeo la picha la YANGA FC
YANGA SC imeanza vyema michuano ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuichapa Mafunzo FC mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mshambuliaji Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma alifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na mshambuliaji mpya, Paul Nonga akaingia mwishoni mwa kipindi cha pili na kufunga bao katika mpira wa kwanza kugusa.


Mafunzo waliuanza vizuri mchezo wa leo na dakika ya kwanza tu mshambuliaji wake Sadikc Habib alikaribia kufunga kama si shuti lake kuokolewa na kipa Deo Munishi ‘Dida’.


Ngoma akaifungia Yanga SC bao la kwanza dakika ya 31 akimalizia krosi ya Mzimbabwe mwenzake, Thabani Scara Kamusoko aliyemtoka vizuri beki wa Mafunzo kulia. 


Dakika mbili baadaye, Ngoma tena akafunga bao akimalizia pasi ya Kamusoko tena, aliyemtoka beki upande wa kulia wa boksi na hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0. 


Tokeo la picha la DONALD NGOMA YANGA FC 
Kipindi cha pili, Yanga SC walianza kucheza kwa kuwadharau wapinzani, hivyo kuwasogeza kwenye eneo lao na dakika ya 81 Mafunzo wakapoteza nafasi nzuri ya kupata bao, baada ya Dida kupangua mkwaju wa penalti wa Kheri Salum. 

Penalti hiyo ilitolewa na Refa Mfaume Ali baada ya Shaaban Ali kukwatuliwa na beki wa Yanga SC, Kelvin Yondani ndani ya boksi.

Paul Nonga aliyeingia dakika ya 88, aliifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 89 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Khalid Mahadhi, kufuatia shuti la Godfrey Mwashiuya aliyeingia pia dakika za lala salama.


Mchezo wa pili wa Kundi B utafuatia Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Amaan, Azam FC wakimenyana na Mtibwa Sugar, wakati kesho kutakuwa na mechi za Kundi A, kati ya JKU na URA Saa 10:15 jioni na Simba SC, mabingwa watetezi dhidi ya Jamhuri Saa 2:15 usiku.


Kikosi cha Yanga SC kilikuwa;
Deogratius Munishi ‘Dida’, Mbuyu Twite, Juma Abdul, Oscar Joshua, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani, Simon Msuva/Malimi Busungu dk88, Thabani Kamusoko/Jerome Sina dk70, Amissi Tambwe/Paul Nonga dk88, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Geofrey Mwashiuya dk70.


Mafunzo FC: Khalid Mahadhi, Juma Mmanga, Samih Nuhu/Haji Ramadhani dk58, Kheri Salum, Hassan Juma/Haji Abdi dk66, Abdul Hassan, Ali Juma/Jermaine Seif dk72, Sadick Habib/Shaaban Ali dk58, Mohammed Abdul na Ali Mmanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox