Premier League imezidi kushika umaarufu wa juu kutokana na kiwango kikubwa cha malipo ya haki za TV nje ya England.
Kwa
sasa Premier League kupitia msimu wa 2016 hadi 19 itaweza kuingiza hadi
paunik bilioni 3.2 wakati wakati inaanza kujulikana kwa jina hilo msimu
wa 1992-93 ilikuwa inaingiza kitita cha pauni milioni 8 tu kwa haki za
kuonyeshwa kwa dunia nzima.
Marekani
ndiyo wanaonekana kulipa fedha nyingi zaidi kwani watatoa hadi pauni
milioni 109.6 wakifuatiwa na nchi za Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la
Sahara, Tanzania ikiwa ndani ambao wanamwaga pauni milioni 98.6.
Umaarufu
wa ligi hiyo umekuwa ukizidi kupaa kwa kasi na kuchangia kuziongezea
klabu hizo kiwango kikubwa cha faida kupitia haki hizo za uonyeshaji wa
mechi za Ligi Kuu England.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni