Timu ya taifa ya Chad imejiondoa kwenye mashindano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika, AFCON kwa mwaka 2017 nchini Gabon.
Chad iliyokuwa imepangwa kundi G lenye timu za Tanzania, Nigeria na Misri imelazimika kujiondoa mashindanoni sababu kubwa ikiwa ni ukosefu wa fedha uliolikumba taifa hilo.
Katika barua yake iliyotumwa kwa Shirikisho la kandanda la Tanzania, Chad imeelezea ‘ukata’ unaowakabili hali iliyopelekea kushindwa kusafiri kutoka nchini kwao kufika Jijini Dar es salaam.
Kiukweli, nchi yetu inapitia kipindi kigumu cha matatizo ya uchumi na kwa upana ushiriki wetu kwenye mashindano mbalimbali umekuwa wa kuishia njiani kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Ilieleza taarifa iloyopo kwenye barua hiyo.
Chad inajitoa baada ya kukamilisha mechi tatu za mzunguko wa kwanza, ikifungwa zote 2-0 na Nigeria ugenini, 5-1 na Misri nyumbani na 1-0 na Tanzania nyumbani Jumatano.
Sasa Kundi G linabaki na timu tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Misri. Chad hawajaja Tanzania na maana yake mechi ya kesho na Taifa Stars haitakuwepo, lakini bado CAF haijatoa taarifa yoyote juu ya hilo.
Mpaka sasa, Chad inashikilia mkia kwenye kundi lao ikiwa haina alama hata moja huku Misri ikiongoza kundi hilo ikiwa na alama 7 ikifuatiwa kwa ukaribu na Nigeria yenye alama 5 na Tanzania ikiwa na alama 4.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Jijini, D,njamena nchini Chad kati ya Tanzania ulimalizika kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 huku nahodha mpya wa Tanzania, Mbwana Samatta akikiongoza vizuri kikosi chake kwa kuwa ndiye aliyefunga bao hilo pekee lililoipa ushindi Tanzania.
Chad inajitoa baada ya kukamilisha mechi tatu za mzunguko wa kwanza, ikifungwa zote 2-0 na Nigeria ugenini, 5-1 na Misri nyumbani na 1-0 na Tanzania nyumbani Jumatano.
Sasa Kundi G linabaki na timu tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Misri.
Chad hawajaja Tanzania na maana yake mechi ya kesho na Taifa Stars haitakuwepo, lakini bado CAF haijatoa taarifa yoyote juu ya hilo.
BAADA YA KUJITOA
Kujitoa kwa Chad katika mechi za kuwania kucheza Afcon huenda likawa jambo jema.
Kwa hali ilivyo, kila timu italazimika kudondosha pointi moja kutoka katika Kundi G iliyopo Stars.
Hivyo, Stars yenye pointi 4, itabaki na pointi moja tu, Nigeria itabaki na pointi mbili huku Misri ikibaki kileleni na pointi 4.
Jambo
hilo linapoteza kabisa matumaini ya Taifa Stars huku ikiacha matumaini
makubwa kabisa kwa Misri hasa kama itashinda mechi yake dhidi ya
Nigeria, keshokutwa.
Kama Misri itashinda, basi itakuwa imefuzu kucheza Afcon kwa asilimia 95.
Tayari
Stars ilikuwa imecheza mechi tatu, ilianza kwa kupoteza dhidi ya Misri
ugenini, ikatoka sare ya bila mabao na Nigeia jijini Dar es Salaam kabla
ya kushinda kwa bao 1-0 mjini ND'jamena dhidi ya wenyeji Chad ambao
wamejitoa kwa madai hawana nauli.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni