TIMU
ya taifa ya Nigeria imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Misri
katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika leo mjini
Kaduna.
Mashabiki takribani 40,000 walishuhudia mchezo huo katika uwanja wa Ahmadu Bello uwanja ambao unauwezo wa kuchukua watazamaji 25,000
Oghenekaro Etebo alianza kuifungia Nigeria dakika ya 60, akimalizia mpira uliorudi baada ya kufonga mwamba kufuatia shuti la Kelechi Iheanacho.
Oghenekaro Etebo (alienyanyua mikono juu)
Hata hivyo, Mohammed Salah akaisawazishia Misri dakika ya mwisho na kuwazima mashabiki wa nyumbani.
Misri wakishangilia goli la Mohamed Salah
Sare
hiyo inaifanya Misri ifikishe pointi saba na kuendelea kuongoza kundi
hilo, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi tano sasa, wakati Tanzania
iliyoifunga Chad mjini D'jamena Jumatano ni ya tatu kwa pointi zake nne.
Nigeria na Misri zitarudiana mjini Alexandria Jumanne, wakati Tanzania na Chad zitarudiana Dar es Salaam Jumatatu.
Ikumbukwe mshindi wa kundi tu ndiye atafuzu kwa fainali za mwakani za AFCON nchini Gabon.
Ikumbukwe mshindi wa kundi tu ndiye atafuzu kwa fainali za mwakani za AFCON nchini Gabon.
Iwobi akiingia kuchukua nafasi ya Moses Simon
Mabingwa watetezi nao, Ivory
Coast wamepata ushindi wa kwanza Kundi I baada ya kuilaza 1-0 Sudan
Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, bao pekee la Gervinho
dakika ya 34.
Tembo wa Ivory Coast waliotoa sare ya bila kufungana katika mechi zao mbili za mwanzo dhidi ya Gabon na Sierra Leone, sasa wanafikisha pointi tano na kupanda nafasi ya pili nyuma ya Gabon wenye pointi saba, wakati Sudan ni ya tatu kwa pointi zake tatu na Sierra Leone yenye pointi moja inashika mkia.
Matokeo mengine, Algeria imeifunga 7-1 Ethiopia Uwanja wa Mustapha Tchaker, Mali imeifunga 1-0 Equatorial Guinea Uwanja wa Machi 26, Guinea imetoa sare ya 0-0 Malawi Uwanja wa Septemba 28, Tunisia imeifunga 1-0 Togo Uwanja wa Mustapha Ben Jannet, Mauritania imeifunga 2-1 Gambia Uwanja wa Nouakchott na Swaziland imelazimishwa sare ya 1-1 na Zimbabwe.
STORI YA PILI;
Kiungo wa Ufaransa, Paul Pogba (katikati) akiruka juu kupiga mpira katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji Uholanzi mjini Amsterdam usiku wa jana
.
Ufaransa ilishinda 3-2 mabao yake yakifungwa
na Antoine Griezmann, Olivier Giroud na Blaise Matuidi wakati ya Uholanzi yalifungwa na Luuk de Jong na Ibrahim Afellay
STORI YA TATU;
Mshambuliaji
wa Uruguay, Luis Suarez akishangilia baada ya kuifungia timu yake
katika sare ya 2-2 na wenyeji Brazil usiku wa jana Uwanja wa Pernambuco
Arena mjini Recife kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
Bao lingine
la Uruguay lilifungwa na Edinson Cavani, wakati ya Brazil yalifungwa
na Douglas Costa na Renato Augusto.
Ikumbukwe Suarez alikuwa anaichezea kwa mara ya kwanza Uruguay baada ya
miezi 20 ya kutumikia adhabu yake ya kufungiwa kwa kumng'ata Giorgio
Chiellini kwenye fainali za kombe la Dunia mwaka 2014 Brazil
Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji ya Barcelona Suarez na Neymar, wakikumbatiana katika mchezo huo
MATCH FACTS
Brazil:
Alisson 5.5, Alves 6, Miranda 4, David Luiz 3.5, Filipe Luis 5, Gustavo
6, Fernandinho 6 (Coutinho 67, 6), Renato 7.5, Willian 8 (Lima 85),
Neymar 8.5, Douglas Costa 6.5 (R Oliviera 78)
Booked: Neymar, Alves, Luiz
Goals: Douglas Costa 1, Renato 26
Uruguay:
Muslera 6, Fucile 5, Coates 4, Victorino 5.5, A Pereira 5, C Sanchez
7.5 (Stuani 80), Arevalo 6.5, Vecino 6, C Rodriguez 6, Cavani 7, Suarez
8.5
Booked: Suarez
Goals: Cavani 31, Suarez 48
Attendance: 45,010
Referee: Nestor Pitana (Argentina)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni