STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 24 Machi 2016

MSIBA MZITO KATIKA TASNIA YA SOKA DUNIANI............

 The former Holland forward pictured behind the wheel of an Alfa Romeo in 1968

 JOHAN CRUYFF HAYUPO TENA NASI.

Mshindi wa mara 3 wa tuzo ya Ballon d’Or(Mwanasoka wa kwanza kuweka rekodi hii), gwiji wa soka wa vilabu vya Ajax na Barcelona na timu ya taifa ya Uholanzi, alikuwa mwanamapinduzi wa kweli wa mchezo huu wa soka.

CeUIQYOXEAIyyxs
Akiwa anavalia jezi maarufu namba 14 ya Uholanzi aliuwasha moto mkubwa viwanjani na kufanikiwa kuiongoza nchi yake kucheza fainali ya kwanza ya kombe la dunia mnamo mwaka 1974.
 
CeUNOMTW4AAm3FO.jpg_large
Cruyff alikuwa kipngozi wa timu ya Ajax ambayo ilitawala soka la ulaya kwa miaka mitatu mfululizo – kutokea mwaka 1971-1973. CeUIqUJXIAA0O-E

Aliondoka Amsterdam na kwenda kujiunga na Barcelona mwaka 1973 – baada ya kushinda vikombe 8 vya ligi kuu, makombe matano ya kombe la FA ya Uholanzi, Super Cup, Kombe la ulaya mara 3 na  Intercontinental Cup.

Uhamisho wake kwenda Catalonia ulianzisha uhusiano wa maisha baina ya Barcelona na wachezaji kutoka Uholanzi. Alihamia Barcelona kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi wakati huo, kiasi cha dola millioni 2 za wakati huo.

Alifanikiwa kuiwezesha Barcelona kutwaa taji la kwanza la La Liga tangu mwaka 1960, huku katika msimu huo akiiwezsha Barca kuitandika kipigo kizito Real Madrid cha 5-0 katika uwanja wa Santiago Bernabeu. 

Baada ya mchezo huo maelfu ya mashabiki wa Barcelona walioangalia mchezo huo katika TV walimininika kwenye mitaa ya jiji la Barcelona na kuanza kushangilia. Msimu ulipoisha Cruyff alitunukiwa tuzo ya mwanasoka bora wa ulaya (1974).CeUWU6FW4AErLVb.jpg_large
Cruyff aliitumikia Barcelona kutokea 1973 mpaka 1978, akiifungia magoli 48 katika mechi 143. Kwa ujumla kwenye maisha yake ya soka alicheza mechi 514 na kufunga magoli 290.
2a
Baada ya kuondoka Barcelona alienda US, kisha akarejea kucheza Uholanzi lakini hakucheza sana, akaamua kugeukia kufundisha soka, akajiunga na Ajax FC mnamo mwaka 1985, Cruyff alifanikiwa kuiongoza Ajax kushinda ubingwa wa UEFA Cup baada ya misimu miwili. 

Akiwa kocha wa Ajax, Cruyff alifanikiwa kutengeneza mfumo mpya wa soka wa kutengeneza mfumo wa staili ya uchezaji ambayo ilikuja kuipa mafanikio makubwa Ajax siku za mbeleni.

Training_Ajax,_Cruyff_(r)_en_algemeen_directeur_Arie_van_Eijden_tijdens_persconferentieMwaka mmoja uliofuatia, Cruyff alijiunga na Barcelona kama kocha mkuu, na kutengeneza  ‘Dream Team’.
vitrina_10.v1308656252Alipohamia Barcelona, Cruyff akawaleta wachezaji kama Pep Guardiola, José Mari Bakero, Txiki Begiristain, Ion Andoni Goikoetxea, Ronald Koeman, Michael Laudrup, Romário, Gheorghe Hagi, and Hristo Stoichkov.

 Cruyff’s “Dream Team” ilishinda La Liga mara nne kutoka mwaka 1991 mpaka 1994, na pia walifanikiwa kuifunga Sampdoria katika fainali ya kombe la washindi mwaka 1989 na mwaka 1992 katika European Cup katika dimba la Wembley Barcelona ikashinda Copa Del Rey pia mwaka 1990,  European Super Cup 1992 na makombe matatu ya  Supercopa de España huku wakimaliza kama washindi wa pili kwa  Manchester United na A.C. Milan katika fainali mbili za ulaya.

Johan Cruyff (Ajax manager) smokes a cigarette Pic : Action Images

Cruyff anaripotiwa kuwa alikuwa akivuta sigara 20 kwa siku kabla ya kufanyiwa matibabu ya moyo mara mbili mnamo mwaka 1991 wakati akiwa kocha wa Barcelona, baada ya hapo akaacha uvutaji sigara.

 Pia aliongoza kampeni ya kupiga vita uvutaji wa sigara chini ya usimamizi wa idara ya afya ya serikali ya Catalunya.

243759_heroa 
Mpaka anaondoka Barcelona mwaka 1996, Cruyff alikuwa ameshinda makombe 11 na Barcelona, rekodi ambayo ilimfanya uwa kocha mwenye mafanikio zaidi katika klabu hiyo kabla ya mwanafunzi wake wa Pep Guardiola hajavunja rekodi yake kwa kushinda makombe 15.

Mnamo mwaka 1999, Cruyff alipigiwa kura kuwa mwanasoka bora wa karne barani ulaya.

Mdachi huyu alikuwa mwanamapinduzi aliyebuni mbinu nyingi na filosofi zinazoendelea kuleta mabadiliko katika soka leo hii.


                             Atakumbukwa na kamwe hatosahaulika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox