STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumatano, 23 Machi 2016

BAADA YA BARUA YA MANARA BODI YA LIGI KUU YABADILISHA RATIBA ................

VPL-Tanzania

Marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom yamezingatia mechi za viporo za timu za Azam na Yanga zinazoshiriki mashindano ya kimataifa (Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho).


Pia ushiriki wa Azam na Yanga katika mechi zijazo za mtoano (play offs) zinazokutanisha timu zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, na zile zilizosonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho.

Iwapo Azam itasonga mbele itacheza mechi hizo za mtoano, wakati Yanga yenyewe itacheza tu mechi hizo za mtoano iwapo itatolewa katika raundi inayofuata ya Ligi ya Mabingwa.

 Hivi sasa Azam na Yanga zinashiriki hatua ya 16 bora ambayo itachezwa kati ya Aprili 8-10 kwa mechi za nyumbani, na Aprili 19 na 20 kwa mechi za ugenini.

Mechi za kwanza za raundi ya mtoano (play offs) zitachezwa kati ya Mei 6-8 wakati za marudiano zitafanyika Mei 17-18. 

Yanga ikiitoa Al Ahly maana yake haitacheza hatua ya mtoano (play offs), na badala yake itasubiri moja kwa moja hatua ya makundi ambayo mechi zake za kwanza zitafanyika kati ya Juni 17-19.

Marekebisho mengine yanaweza kufanyika kwa kuzingatia matokeo ya scenario hizo hapo juu.
Wasalaam,

Boniface Wambura
Ofisa Mtendaji Mkuu
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB)
Ratiba kamili inasomeka hivi…
Ratiba-marekebisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox