Tuangalie namna Muargentina huyu alivyofikisha idadi hii ya magoli kwa klabu na nchi yake.
Messi huanza mechi taratibu
Messi ni aina ya wqchezaji ambao huanza mechi taratibu, takwimu zinaonyesha ni magoli 50 tu kati ya 500 ambayo alifunga katika dakika 15 za kwanza za mechi – lakini amekuwa mwiba kwa timu pinzani kwa dakika nyingine 75 zinazofuatia. Huadhibu sana timu pinzani pale zinapoanza kuchoka.
Ni mguu mmoja tu wa Messi ambao ni hatari
Unataka kumzuia Messi asifunge? Mzuie asipige na mguu wake wa kushoto, unaweza kufanikiwa kwa asilimia 81%, kwa sababu asilimia 81 ya magoli yote aliyofunga amefunga na mguu wa kushoto – magoli 406, wakati mguu wa kulia magoli 71, na kichwa magoli 21. Mipira ya adhabu ndogo – magoli 25 na penati 64.
Kwenye misimu 8 iliyopita amefunga wastani wa magoli 40 kwa msimu.
Messi msimu huu mpaka sasa amefikisha magoli 42.
Timu alizozifunga
Atletico Madrid na Sevilla wana sababu za kumuogopa Messi zaidi – amezifunga magoli 25 kila timu. Magoli manne zaidi ya aliyoyafunga dhidi ya Real Madrid.
Mashindano aliyofunga magoli
Magoli mengi zaidi amefunga katika La Liga. Wakati kwenye World Cup amefunga matano tu.
Amezidiwa na Cristiano Ronaldo
Messi pamoja na mpinzani wake Ronaldo wamefunga jumla ya magoli 1,039.
Anahitaji kumpa zawadi Dani Alves
Barcelona right-back Dani Alves ndio anaongoza kumpa Messi pasi za mwisho kabla ya kufunga, wamecheza pamoja kwa miaka 10.
Messi alifanikiwa kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli matano katika mchezo mmoja wa Champions League wakati Barca ilipoifunga Bayer Leverkusen 7-1 mwaka 2012.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni