
Toto Africans ya mkoani MWanza wamewazuia Simba SC kurejea kileleni hii leo baada ya kuifunga Simba SC goli 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom, ikiwa ni mchezo wa pili mfululizo Simba SC wakipoteza.
Kabla ya mchezo wa leo Simba SC walipoteza mbele ya Coastal union katika mchezo wa kombe la TFF, na leo wamepoteza tena mbele ya Toto Africans katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo wa leo Simba SC walitawala mchezo lakini walikosa mbinu ya kujaza mpira kwenye nyavu za Toto African na wakati Toto African muda mwingi wakiwa wanajilinda na kupeleka mashambulizi ya kushtukiza.
Alikuwa Waziri Junior aliye waliza Simba SC katika dakika ya 21 kwa ashuti la mit 24 akimalzia mpira aliotengewa na Edward Christp[her kwa kichwa na Wazir kuindikia Toto goli pekee la ushindi hii leo.
Katika kipindi cha kwanza koca wa Simba SC Jackson Mayanja alizawadiwa kadi nyekundu na kupelekea kuondolewa katika benchi.

KAtika kipindi ca pili dakika ya 47 beki Hassana Kessi wa Simba SC alizawadiwa kadi nyekundu na kupeleka Simba SC kumaliza wakiwa pungufu uku wakikubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Toto Africans.
Hassan Kessy baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu |
MSIMAMO WA LIGI KUU BAADA YA MCHEZO WA LEO
Rn | Timu | P | W | D | L | F | A | Gd | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | YANGA | 24 | 18 | 5 | 1 | 57 | 13 | 44 | 59 |
2 | SIMBA SC | 25 | 18 | 3 | 4 | 43 | 14 | 29 | 57 |
3 | Azam FC | 24 | 16 | 7 | 1 | 41 | 16 | 25 | 55 |
4 | MTIBWA SUGAR | 26 | 12 | 7 | 7 | 29 | 19 | 10 | 43 |
5 | T. PRISONS | 26 | 10 | 11 | 5 | 23 | 21 | 2 | 41 |
6 | MWADUI FC | 26 | 9 | 7 | 10 | 25 | 25 | 0 | 34 |
7 | STAND UNITED | 25 | 10 | 4 | 11 | 22 | 22 | 0 | 34 |
8 | NDANDA FC | 27 | 7 | 12 | 8 | 26 | 27 | -1 | 33 |
9 | MAJIMAJI FC | 26 | 9 | 6 | 11 | 20 | 34 | -14 | 33 |
10 | MBEYA CITY | 26 | 8 | 6 | 12 | 28 | 33 | -5 | 30 |
11 | TOTO AFRICANS | 27 | 7 | 9 | 11 | 25 | 36 | -11 | 30 |
12 | KAGERA SUGAR | 27 | 6 | 7 | 14 | 19 | 31 | -12 | 25 |
13 | JKT RUVU | 25 | 6 | 6 | 13 | 24 | 34 | -10 | 24 |
14 | MGAMBO SHOOTING | 26 | 5 | 8 | 13 | 20 | 32 | -12 | 23 |
15 | AFRICAN SPORT | 27 | 6 | 5 | 16 | 11 | 30 | -19 | 23 |
16 | Coastal Union | 27 | 5 | 7 | 15 | 16 | 37 | -21 | 22 |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni